Minyoo ni viumbe hai
ambavyo husababisha madhara ya kiafya kwa mtu aliyeambukizwa.minyoo huishi na
kukua katika utumbo ambamo hufyonza virutubisho ambavyo ni muhimu kwa lishe ya
binadamu.aina ya minyoo inayosababisha kichocho huishi katika kibofu cha mkojo.
Minyoo kwenye utumbo
huchangia kwa kiasi kikubwa katika kudhoofisha lishe ya binadamu,hupunguza
uwezo wa mtu wa kufanya kazi,udumavu wa akili na madhara mengine. Minyoo ya
tumbo inayomwathiri mwanadamu ni pamoja na minyoo mviringo.minyoo ya safura,minyoo
mjeledi,ninyoo sindano,minyoo uzi na tegu.
Dalili za uambukizo wa
minyoo ya kwenye utumbo ni:
1. Kuwashwa mwili na sehemu ya haja kubwa.
2. kukohoa kikohozi kikavu
3. kukosa hamu ya kula
4. kuumwa tumbo na wakati mwingine
kuharisha.
5. Udhaifu wa mwili na kuckoka kwa mara kwa
mara
6. Kuvimba tumbo.
7. Kutapika
8. Utumbo kutoka nje ya unyeo
9. Kutoa minyoo kwa njia ya haja kubwa,
kutapika minyoo au minyoo kutoka puani.
10. Kizunguzungu
11. Kupauka kwa fizi, ulimi na utando wa
macho.
12. Kuvimba miguu.
Aidha kuna athari
zinazosababisbwa na minyoo kwenye utumbo kama vile udhaifu wa mwili, utumbo
kuziba, kuumwa tumbo, kudumaa kiakili, utapiamlo, upungufu wa wekundu wa damu
mwilini na kifo.
Minyoo huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda
kwa mwingine kwa njia mbalimbali kama vile kula kinyesi cha mtu aliyeathirika
kupitia chakula,maji, udongo au matunda, kutonawa mikono baada ya kutoka
chuoni. Njia nyingine ni maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto aliye
tumboni.
Ili kujilinda na minyoo
tunashauriwa kudumisha usafi haswa usafi binafsi kwa maana ya kunawa mikono kwa
sabuni mara baada ya matumizi ya choo na kabla ya kushika chakula, kuosha
kikamilifu matunda, mboga za majani na vyakula, kupika nyama vizuri ili kuuwa
minyoo inatokaa katika nyamaa, mama mjamzito kuhudhuria clinic na kupatiwa dawa
za kujikinga yeye na mtoto dhidi ya minyoo . watoto chini ya miaka mitano
kuhudhuria clinic ili kupatiwa dawa ya kujilinda na minyoo kikamilifu.
Tanzania bila minyoo
inawezekana kama tutazingatia ushauri wa wataalamu wa afya.
No comments:
Post a Comment