WANAFUNZI WANAOTUMIA UGORO WAKO HATARINI KUPATA SARATANI YA KINYWA


Maelfu ya wanafunzi wako hatarini kupata saratani za vinywa (Oral cancers) kutokana na kuongezeka kwa matumizi holela ya Ugoro (Snuff), Ongezeko la matumizi ya ugoro linakuja baada ya Wizara ya afya na ustawi wa jamii kupiga marufuku uuzaji wa Kuberi.

Akiongea na Daily news, mkuu wa kitengo cha afya ya akili na madawa ya kulevya wizarani, Dk norman Sabuni alisema kwamba kutokana na uchunguzi walioufanywa ulibaini kwamba matumizi ya ugoro yameongezeka na wasambazaji wakuu wakiwa ni walinzi wa Kimasai.
Alisema kwamba “tunajua idadi ya shule ambazo zimawafukuza walinzi wa kimasai baada ya kugundua kwamba wamekuwa wakiuza Tumbaku kwa wanafunzi. Tumbaku ni halali nchini hivyo tunachokifanya ni mwendelezo wa kuwaonya watu juu ya madhara ya matumizi ya tumbaku”.

Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi aliliambia gazeti hilo kwamba hana  taarifa kama kuna wanafunzi wanaotumia Ugoro na kuapa kwamba iwapo taarifa zitafika mezani kwake basi atachukua hatua stahiki.

Dk Sabuni alithibitisha kwamba wanafunzi wengi wanapendelea ugoro kuliko sigara kwasababu ugoro hauachi harufu baada ya kuutumia na unalewesha haraka ukilinganisha na Sigara. Aliongeza kwamba wanafunzi wengi hawautumii ugoro kwa kuuvuta kupitia pua kwakuwa wanaogopa kupiga chafya hivyo hutumia njia ya kinywa hali ambayo huwapelekea kulewa mapema kutokana na kiasi kikubwa cha ugoro kuingia kwenye mzunguko wa damu kwa kutuama kwenye lips za ndani ya domo.

Mtaalamu huyo alisema Matumizi ya Ugoro yanaweza kupelekea Saratani za lips, mdomo, koo, ulimi na hata kuathirika mfumo wa akili (mental disorders).

Muuzaji ugoro wa kimasai wa Mwenge aliliambia gazeti hilo kwamba sio kazi yao kujua mnunuaji yupi ni mwanafunzi na yupi sio mwanafunzi kwasababu wanunuzi huwa hawavai sare za shule wanapoenda kununua. Aliongeza kwamba, licha ya kuona kuwa watumiaji wengi ni vijana wadogo lakini pia amegundua kwamba watu kutoka mikoa mingine wamekuwa wakitumia Ugoro kwa wingi ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo ni wamasai pekee ndio waliokuwa wameteka matumizi hayo.

Mudi Chokora (20), mtumiaji wa Ugoro kwa miaka mingi alililiambia gazeti hilo kwama mapenzi yake kwenye Ugoro yalianza kwa kuonja kwa walinzi wa kimasai waliokuwa wanaishi jirani na baada ya kipindi kifupi akajikuta amezamia kwenye matumizi ya Ugoro. Aliongeza kwamba ukilinganisha na Sigara ambazo gharama zake hupanda kila mwaka, Ugoro sio tu gharama nafuu lakini pia haihitaji kupiga mswaki mara kwa mara kwa kuwaogopa kushtukiwa na wazazi.


Kujua zaidi bofya HAPA







No comments:

Post a Comment