Ugonjwa wa mfumo wa mkojo kitaalamu
urinary tract infection(UTI) umekuwa ukisumbua watu wengi. Vimelea
vinavyosababisha ugonjwa katika mfumo wa mkojo hukua na kusambaa endapo kinga
ya mwili inakuwa ndogo hivyo makundi yaliyo katika hatari ya magonjwa haya ni
watoto chini ya miaka mitano, wamama wajawazito, wanawake na watu wote wenye
upungufu wa kinga.
Mlezi au mzazi anaweza kuzuia maambukizi
ya ugonjwa huu kwa watoto kwa kufanya yafuatayo;
1. Hakikisha matumizi sahihi ya dawa za
kuzuia bacteria(antibiotics) kwa watoto kama vile amoxylin na cephalosporin
pale unapoandikiwa na mtaalamu wa afya.matumizi yasiyo sahihi ya dawa hizi
yanaweza kumuweka mtoto katika hatari zaidi ya kupata maambukizi.pale
unapoandikiwa dawa hizi hakikiksha unampa mtoto kwa wakati husika na dozi
sahihi na usizidishe muda wa matumizi bila ushauri wa daktari.
2. Hakikisha mtoto anakunywa maji mengi kwa siku
kulingana na umri wake.mtoto wa miaka 3 na kuendelea anashauriwa kunywa maji
glass 6 mpaka 8 kwa siku ili kuepuka
upungufu wa maji mwilini(dehydration) hali inayomweka katika hatari zaidi ya
kupata maambukizi ya mfumo wa mkojo.
3. Njia sahihi ya kumsafisha mtoto wa kike
sehemu za siri ni kutoka mbele kwenda nyuma ili kuepuka kusambaza bacteria wa
njia ya haja kumbwa maarufu kama normal flora ambao kwa kawaida wakitoka katika
njia ya haja kubwa kwenda katika njia ya mkojo wanasababisha ugonjwa katika
mfumo wa mkojo. Kwa mtoto ambaye ameanza kunawa mwenyewe hakikisha unamfundisha
njia sahihi ya kunawa ili kuepuka maambukizi. Kwa mtoto wa kiume hakikisha
anatahiriwa mapema ili kuepusha hatari ya maambukizi ya ugonjwa huu na kwa Yule
ambaye hajatahiriwa bado hakikisha unamsafisha ndani ya ngozi ya uume wa mtoto
mara kwa mara kuepuka kukua kwa bacteria katika mfumo wa mkojo. Na endapo mtoto
ameanza kunawa mwenyewe hakikisha unamfundisha njia sahihiya unawaji.
4. Epuka matumizi ya sabuni kali zenye
kemikali kwa mtoto ambazo zinaweza
kupelekea muwasho unaoweza kusababisha michubuko
katika sehemu za siri hali
inayorahisisha maambukizi ya vimelea vya magonjwa ya mfumo wa mkojo.
5. Hakikisha mtoto havai nguo zinazombana
sana katika maeneo ya siri kwa kumvalisha nguo zinazoruhusu hewa kupita ili
kuzuia joto na unyevunyevu unaoengeneza mazingira mazuri kwa ukuaji wa vimelea vya magonjwa katika mfumo wa
mkojo.
6. Hakikisha mtoto anakojoa mara kwa mara
na hakai na mkojo kwa muda mrefu.
7. Kama mtoto atakuwa na dalili ya ugonjwa wa mfumo
wa mkojo kama vile homa, maumivu wakati wa kukojoa, mkojo wenye mawingu na unaotoa harufu kali mpeleke
mapema katika kituo cha afya nahakikisha unatumia kwa usahihi dawa
alizoandikiwa. Usitumie dawa zozote bila
ushauri wa daktari.
Source: Click HERE
No comments:
Post a Comment