KUISHI NDANI YA ‘KIPUPWE’ SIO SIFA, JITATHIMINI!



Kuna utamaduni mbaya ambao umekuwa ukijengeka nchini kwa walio wengi kwamba kuishi au kufanya kazi kwenye nyumba au ofisi yenye upepo unaotokana na kifaa cha Air condition (AC) au Kiyoyozi au ‘Kipupwe’ kama wengi wanavyopenda kukiita ni ‘SIFA’ na kinamfanya mtu kuonekana wa hadhi ya juu kwenye jamii na hivyo kuwavutia watu wengi kumiliki na kutumia kifaa hicho.

Pamoja na sifa zote hizo lakini swali ni Je, matumizi ya kifaa hiki cha AC yana madhara gani kiafya?

Tafiti mbalimbali zilizofanyika ulimwenguni zimebainisha madhara kadhaa ya kiafya yanayoweza kutokea kwa mtu anaetumia ‘Kipupwe’ kwa muda mrefu, yafuatayo ni baadhi ya madhara hayo:



1. AC HUATHIRI MFUMO WA HEWA

‘vipupwe’ hutengeneza majimaji kwenye koili za ndani ya AC ambayo hutengeneza mazingira mazuri kwa bacteria na fangasi (molds) kukua na kusambaa ndani ya chumba. Bacteria na fangasi hawa huaribu mfumo wa hewa kwa watumiaji vipupwe na kusababisha magonjwa ya Asthma na bronchitis, maambukizi ya mapafu, aleji, chafya za mara kwa mara n.k.

2. AC HUONGEZA  VICHAFUZI VYA NDANI (INDOOR AIR CONTAMINANTS)

Vipupwe huongeza wingi wa vichafuzi (pollutants) kama vile bacteria, molds, virusi, pollen na vijidudu vidogo kutoka kwenye mazingira ya nje kwenda ndani ya nyumba, hali hii inaweza kuleta madhara makubwa kwa watu ambao tayari wana matatizo ya mfumo wa hewa na matatizo ya moyo, pamoja na kuwaathiri watu wenye kinga ya chini ikiwemo wazee na watoto wadogo, kwakuwa watu hawa hutumia muda wao mwingi wakiwa ndani ya nyumba.

3. AC HUONGEZA MAAMBUKIZI YA MAGONJWA

Utafiti uliofanywa baada ya tukio la kusambaa kwa ugonjwa wa Legionnaire katika hospitali ya Tenn uingereza mwaka 1980 ambapo watu 44 waliambukizwa ugonjwa huo, umebaini kwamba AC za mfumo wa Kati (Cental air conditioning) zilihusika na kusambaa kwa bacteria wa Legionnaire pneumophila baina ya wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika hospitali hiyo, bacteria hao walikutwa kwenye maji ya kupooza hewa ndani ya AC na hivyo kudhihirisha kwamba AC zinaweza kusambaza magonjwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

4. AC HUPUNGUZA UTENDAJI KAZI MAOFISINI

Katika utafiti uliochapishwa kwenye jarida la “International Joural of Epidermiology’, tarehe 19, Aug, 2004 ulionyesha kwamba watu wanaofanya kazi kwenye kwenye ‘kipupwe’ huwa wana dalili nyingi za magonjwa kama vile kuumwa kichwa, kuchoka, kuirritate mucous membrane, kupata shida ya kupumua, na kuathirika ngozi, na kushindwa kufanya kazi zao kwa ufasaha ukilinganisha na watu wanaofanya kazi katika majengo yenye mzunguko mzuri wa hewa yasiyo na ‘kipupwe’. Hali hii ilibatizwa jina na mamlaka ya ulinzi wa mazingira ya Marekani (EPA) na kuitwa “Sick Building Syndrome” ikimaanisha kwamba dalili za magonjwa zinazotokea kwenye idadi kubwa ya watu wanaingia kwenye jengo la ofisi lakini wanapotoka tu kwenye jengo hilo dalili hizo za magonjwa zote hutoweka.

Kutokana na madhara hayo kama yalivyoainishwa hapo juu nadhani utakubaliana na mimi kwamba kuishi au kufanya kazi kwa muda mrefu ndani ya ‘Kipupwe’ sio SIFA bali ni MAJANGA, tunashauriwa kujenga nyumba zetu za kuishi na ofisi zenye madirisha makubwa yenye uwezo wa kuruhusu mzunguko bora wa hewa.

Kwa viwango vya hapa nchini, ukubwa wa madirisha unatakiwa kuwa angalau 1/8 ya eneo la chumba (floor area) pia umbali kutoka uzio au jengo moja hadi jingine unapashwa kuwa angalau mita 3 hadi 5 ili kuruhusu hewa kupita kwenye kila jengo. Pamoja na viwango vivyo lakini pia tunashauriwa kujenga uzio mfupi usiopita urefu wa madirisha, kutochanganya majengo ya Maghorofa na majengo ya floo moja kwenye ploti moja ili kuepuka kuuzuia upepo kutofikia majengo mengine na kuzingatia mpangilio mzuri wa vitu vya ndani ya nyumba ili kuekupa mbanano usiokuwa wa lazima unaoweza kuzuia mzunguko wa hewa ndani ya nyumba.


Kusoma zaidi BOFYA HAPA



3 comments:

  1. Husababisha pia social conflicts hasa kwenye ofisi ambazo wanashare watu wengi. Hapo lazima atajitokeza mmoja kati yao atakuwa anaseti AC kwenye baridi kali na kulazimisha wengine washinde wanatetemeka na kuvaa makoti kila siku. Misuse ya of technology.

    ReplyDelete
  2. Kabsa.binafsi I hate AC.or unapungua,mwenxio anaongeza.daah!lzm mvutano utokee.me,navaa kot kbsa ofisin

    ReplyDelete