ABOUT US


'AFYA YA MAZINGIRA' ni tovuti ya kitaalamu yenye lengo la kupasha habari na kutoa elimu kwa jamii yetu ya kitanzania na Afrika kwa ujumla juu ya uhusiano wa Afya zetu na Mazingira yanayotuzunguka ili kuhamasisha uboreshaji wa Afya zetu kwa kuepuka Magonjwa na madhara mengine ya Kiafya yanayosababishwa na mazingira hatarishi.

Dhamira ya kuanzishwa na kuiendeleza tovuti hii imekuja baada ya kuona kuna ongezeko kubwa la milipuko ya magonjwa na majanga mengine ya kiafya yanayozikumba nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, magonjwa na majanga haya kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na watu kukosa elimu na maarifa ya kutosha ya kuweza kutengeneza mazingira rafiki ya kuishi na kujikuta wanatengeneza mazingira mabaya ambayo huvutia vimelea hatari vya magonjwa kukua na kuongezeka na hatimaye kuleta milipuko mipya ya magonjwa au kujirudia kwa miripuko ya kale ambayo iliaminika kwamba imetokomezwa.

Mbali na vimelea vya magonjwa lakini pia kazi tunazofanya, vyakula tunavyokula, tamaduni zinazotuzunguka, makazi tunayoishi na maendeleo tunayopitia yamekuwa yakiathiri afya zetu kwa kiasi kikubwa bila ya sisi kujijua, na kwasababu KINGA ni bora kuliko TIBA, swali linakuja ni nani atakayeweza kumkinga huyu asiyejua!? jibu ni moja kwamba ni wale waliopewa dhamana ya kuelimishwa ili walisaidie Taifa hivyo hata wewe baaada ya kuelimika kwa kupitia machapisho ya tuvuti hii bado una jukumu la kufanya la kuelimisha jamii yako.

Machapisho ya tovuti hii yanachapishwa na wataalamu wa kada ya Afya ya Mazingira kwa mujibu wa taaluma ya Afya ya mazingira (Environmental Health Sciences), na vyanzo mbalimbali vya habari zenye uhakika vinatumika ili kutimiza lengo la kumpasha habari na kumuelimisha mtanzania kwa kiwango kinachohitajika ili kumkinga na hatari yoyote ya kiafya inayoweza kujitokeza.

Aidha 'AFYA YA MAZINGIRA' inachukua nafasi hii kumkaribisha kila mtu kusoma, kuchangia, kukosoa na kurekebisha chochote kinachojitokeza kwenye machapisho yanayochapishwa kwenye tovuti hii, pia inapokea habari na makala yoyote inayohusu kada ya afya ya mazingira bila malipo yoyote ili ipitiwe na kuchapishwa katika tovuti hii kwa lengo la kumpasha habari na Kumelimisha Mtanzania na watu wa mataifa mengine.



AFYA YA MAZINGIRA
"Jamii yenye afya bora na kinga madhubuti dhidi ya Magonjwa"



4 comments:

  1. It sound very cool to me, this is true Tanzanian patriotism we were talking about. Nice job!

    ReplyDelete
  2. HONGERA SANA TUPO PAMOJA!

    ReplyDelete