Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa nchini Marekani (FDA) imewatahadharisha watumiaji wa Vidonge vya kuongeza vitamin
B mwilini ambavyo hujulikana kama B-50 kuwa vimetengenezwa kwa kujumuisha
kemikali mbili hatari za anabolic steroids (Steroids methasterone na
dimethazine) ambazo husababisha ukuaji hafifu wa nywele kwa wanawake na
upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume.
FDA imesema kwamba
bidhaa hiyo imekuwa ikiuzwa bila kuonesha viambata hatari vya steroids kwenye
lebo ambavyo kimsingi havirususiwi kuwepo kwenye vidonge hivyo.
Hata hivyo FDA imesema
imepokea ripoti 29 za madhara ya matumizi ya vidonge hivyo ikiwemo Uchovu (fatigue),
kukakamaa kwa misuli (Muscle cramping) na maumivu ya misuli (muscle pain). Wanawake
waliotumia vidonge hivyo wameripoti kupatwa na ukuaji wa nywele usio wa kawaida
na kukosa siku zao. Wanaume waliotumia vidonge hivyo wameripoti kupungukiwa na
nguvu za kiume na vichocheo vya kiume (testosterone).
Kusoma zaidi bofya HAPA
No comments:
Post a Comment