Utafiti uliofanywa
nchini Ufaransa na timu ya wataalamu kutoka chuo kikuu cha Havard kitivo cha
afya ya jamii ikiongozwa na Dr. Marc G. Wesskopf kutoka idara ya Afya ya
Mazingira chuoni hapo, umeonesha kwamba sumu za kuulia wadudu mashambani (pesticides)
zilizotengenezwa kwa kemikali za sumu zinazojulikana kwa kitaalamu kama
Organophosphate, zinazoweza kuathiri
mfumo wa fahamu na kusababisha matatizo ya kiafya ya unyogovu (depression).
Utafiti huo ulifanywa
kwa kufuatilia historia ya wakulima walioajiliwa kati ya mwaka 1998-2000 huko
Ufaransa. Ambapo kati ya wakulima 567 wenye umri wa miaka 37-78, wakulima 83
(14.6%) walilipotiwa kutibiwa ugonjwa wa unyogovu.
Akiongea na shirika la
habari la Reuter, Dr. Wesskopf alisema kwamba wakulima ambao wanatumia sumu za
kuulia wadudu kwa muda mrefu bila vifaa kinga (long exposure) wako hatarini
kupata matatizo ya unyogovu kuliko wale waliotumia kwa muda mfupi, pia wale
wanaopata dozi kubwa ya organophosphate wako hatarini zaidi ya wale wanaopata
dozi kidogo (dose-response relationship).
pamoja na matokeo hayo
lakini utafiti huo umekosolewa na Mtafiti wa chuo kikuu cha jimbo la Colorado
kuwa haukuangalia uwezekano wa kwamba wakulima wanaotumia sumu hizo wanaweza
kupata madhara mengine ya kiafya ambayo yataathiri utendaji wao wa kazi na
hivyo kuwa katika hali ambayo itawapelekea kupata Unyogovu (depression).
kusoma utafiti huo bofya HAPA
No comments:
Post a Comment