Imerekebishwa na kuchapishwa kutoka BBC SWAHILI leo tarehe 09/07/2013
Wagonjwa wawili wameondolewa bughdha ya kutumia madawa ya kupunguza makali
ya ukimwi maishani mwao baada ya kufanyiwa upasuaji na kupandikiziwa uboho wan
binadamu au (Bone marrow), hatua inayosemekana kuondoa virusi vya HIV mwilini
mwao.
Wagonjwa hao ambao
hawajatajwa majina, wameishi na virusi hivyo kwa takriban miaka 30. Wote
walikuwa wanaugua saratani, aina ya lymphoma, ambayo ilihitaji
wafanyiwe upasuaji sehemu ya Uboho au Bone marrow (ndipo celi mpya za biadamu
hutengezwa mwilini na inaaminika kuwa kitovu cha virusi vya HIV mwilini).
Baada ya kufanyiwa
upasuaji huo, hapakuwa na virusi mwilini kwa miaka miwili kwa mgonjwa mmoja
wakati mwingine anaishi kwa miaka minne bila ya virusi kuonekana. Wagonjwa hao
sasa hawatumii tena dawa za kupunguza makali ya ukimwi. Upasuaji huu ulifanyika
kwa wagonjwa hao kwa sababu walikuwa wanaugua saratani iliyohitaji matibabu.
Madaktai waliofanya
utafiti huo katika hospitali ya matibabu ya wanawake ya Brigham nchini
Marekani, wanasema ni mapema mno kuzungumzia uwezekano wa kutibu virusi hivyo
kwani kuna unawezekano vikarejea wakati wowote, na kuongezea kuwa ni
vigumu sana kutibu Ukimwi, kwa sababu virusi hujificha ndani ya DNA ya mtu
na hivyo kusababisha virusi sugu ambavyo haziwezi kutibika. Madawa ya kupunguza
makali ya virusi vya HIV husaidia kudhibiti virusi hivyo ndani ya damu lakini wakati mtu
anapokosa kumeza dawa hizo virusi hurejea tena.
Inasemekana kwamba ni mapema mno kuona upasuaji
huo kama tiba ya ukiwmi, na hata ikiwa itasemekana kuwa tiba basi sio tiba
nzuri kwani ni ghali mno na kwa baadhi ya wagonjwa kuna uwezekano wa kufariki
ikiwa ni kwa asilimia 15 hadi 20% kwa miaka ya kwanza baada ya kufanyiwa
upasuaji.
No comments:
Post a Comment