Hawakukosea wale waliosema kuwa mboga za majani na matunda
ni kinga kwa afya yako. Matunda mengi yana manufaa lakini tango tunasema
limetia fora.
Kwanza linasifika kwa kuwa na vitamin zote unazohitaji kwa
siku. Tango moja lina vitamin B1, B2, B3, B4 na B6, madini ya chuma, potasium
na zinc.
Pili, unapojisikia kuchoka mchana, kula tango moja ambalo
linaweza kukupa nguvu kwa saa kadhaa.
Tatu, ngozi yako inahitaji tango kutoa seli zilizokufa na
makunyanzi. Weka au sugulia vipande vya tango usoni au sehemu iliyoathirika na
utaona maajabu baada ya siku chache.
Nne, unataka kuondoa ‘hangover’ au maumivu makali ya kichwa,
kula tango ambalo lina sukari ya kutosha na vitamin zitakazoweka mambo sawa
mwilini.
Tano, umemaliza kula, unahisi una harufu mbaya mdomoni
nyakati za mchana. Tafuna vipande vya tango na utapata harufu nzuri ya
mdomo.
Sita, midomo imekauka na inauma? Chukua kipande cha tango na
sugulia mdomoni, utaona mabadiliko katika midomo.
Saba, umekosa muda wa kula mchana, kula tango moja bila
kumenya maganda na litaweza kukaa tumboni kwa saa zaidi ya nane.
No comments:
Post a Comment