TANZANIA ni moja ya nchi zilizojaliwa kuwa na
rasilimali nyingi zinazopatikana katika maeneo mbalimbali, rasilimali hizo ni
pamoja na madini ya aina mbalimbali kama vile almasi, dhahabu, tanzanite, makaa
ya mawe, mekyuli na Urani.
Maana ya Urani
Urani ni madini, kwa
kitaalamu hufahamika kama uranium na ni ya kemikali katika kundi la metali
ambapo hutoa mionzi inayoweza kubadilika kwa haraka na kusababisha athari kubwa
kama tahadhari haikuchukuliwa.
Madini haya hupatikana
ardhini, kwenye mawe na kwa kiasi kidogo kwenye maji, kwa Tanzania baadhi ya
kampuni kama vile Mantra (T) Ltd na Uranex (T) Limited zimefanya utafiti katika
maeneo ya Namtumbo (Mkuju River Project), Bahi na Manyoni na kugundua uwepo wa
Madini hayo.
Matumizi ya Urani
1. Urani hutumika kuzalisha nguvu za nyuklia
(nuclear energy) ambazo husaidia kuzalishwa kwa Umeme wa uhakika.
2. Urani hutumika kutengenezea silaha mfano:
risasi (bullets) na mabomu.
3. Uzani atomia 238 ya Urani hutumiwa na
wanasayansi kubashiri umri wa miamba iliyodumu kwa miaka mingi.
Athari za Urani kwenye Mazingira
1. Uchimbaji wa Urani huitaji eneo kubwa la ardhi
hivyo misitu mingi hukatwa na kuharibiwa, viumbe vingi vinavyotegemea misitu (bioanuwai) huweza kuharibiwa
na kupotea kabisa.
2. Pale patakapochimbwa madini hayo hutokea
uchafuzi vyanzo ya Maji (mfano: Mito, Visima na Chemichemi) na hii inatokana na
matumizi ya kemikali kama vile zebaki na tindikali za salfa ambazo hutumika
katika hatua mbalimbali za uchimbaji wa Urani.
3. Uchimbaji wa Urani husababisha migogoro ya
ardhi kwa kuwaondoa au kuwahamisha watu (wafugaji au wakulima) katika maeneo yao
ya Makazi ili kupisha Shughuli za uchimbaji.
Athari za Urani Kiafya
Madini ya urani yanaweza kuingia kwa mwanadamu kwa njia tofauti
ikiwemo kuvuta vumbi liliopo kwenye hewa au kumeza kwa njia ya chakula,maji au
kupenya kwenye mwili (ngozi) kwa kupitia mionzi yake na kusababisha madhara
Kiafya kama ifuatavyo:
1. Urani ni sumu inayoathiri mwili kwa
kusababisha saratani ya figo, ubongo, ini na damu.
2. Urani husababisha magonjwa ya Moyo, watoto
kufia tumboni, kupungua kwa kinga ya mwili, vifo vya watoto, kuharibika kwa
mimba, watoto kuzaliwa na uzito mdogo, kuathiriwa kwa chembechembe za uzazi za
urithi na watoto kuzaliwa na ulemavu wa ubongo.
Jinsi ya kukabiliana na Athari za Urani
1. Tathmini ya Athari za mazingira lazima ifanywe
mapema kabla, wakati na baada ya kuanza kwa shughuli za uchimbaji ili kuandaa njia
sahihi za kujikinga na Athari zitakazojitokeza.
2. Wachimbaji na wananchi wanaoishi jirani na
maeneo ya uchimbaji ni muhimu waelimishwe jinsi ya kukabiliana na athari za
Urani.
Soma zaidi HAPA
This is over-exaggerated! There is rarely epidemiological evidence to support some highlighted claims. If there are no sufficient scientifically proven evidence to some claims then we use the "Precautionary principle". This is how scientific blaming are based! Yet, there is a plan truth that Uranium is weakly radioactive and heavy metal.Therefore, its chemical toxicity supersede the radiological component!As a heavy metals accumulated in Kidney and Heart...Its biological half life is significant..so can damage.....That's all Kunda...Goodluck
ReplyDelete