Taarifa ya awali ya
utafiti wa kubaini chanzo cha mlipuko wa homa ya mafua makali (MERS) ulizozikumba
nchi za mataifa ya mashariki ya kati ikiwemo Saudi Arabia imeonyesha kwamba
wanyama aina ya Ngamia wanashukiwa kuwa ndio chanzo cha virusi (Coronavirus) vinavyosababisha
homa hiyo.
Utafiti huo ulifanywa
kwa kuchukua sampuli za damu za wanyama wanaofugwa (livestock animals) ikiwemo
Ngamia, kondoo, Mbuzi na Ng’ombe, kutoka mataifa mbalimbali. Sampuli hizo
zilipimwa kama zina kinga ya mwili inayopambana na virusi hivyo (antibodies)
ili kujua kama wanyama hao waliwali waliwahi kutengeneza kinga ya mwili baada ya kuathiriwa na Kirusi hicho kipindi
cha nyuma kabla ya virusi hivyo kusambaa kwa binadamu.
Baada ya vipimo hivyo
matokeo yalionyesha kwamba ngamia 15 kati ya 105 kutoka Visiwa vya Canari
(Canary Islands) walikuwa na kiasi kidogo cha kinga ya mwili inayopambana na
virusi vya Coronavirus, huku Ngamia wote 50 kutoka Oman wakionyesha kubeba
kinga ya mwili ya kupambana na virusi kwa kikubwa hali inayoonyesha kuwa kuna maambukizi
yanayoendelea kutokea baina ya ngamia na kumuathiri binadamu.
Pamoja na matokeo hayo
kuonyesha kwamba ngamia wote kutoka Oman waliwahi kuambukizwa virus vya
Coronavirus lakini hakuna kesi yoyote ya homa ya mafua makali iliyowahi kuripotiwa
kutokea kwenye nchi hiyo hali inayoashiria kwamba huenda maambukizi hayo ni
mampya na huenda nchi hiyo ikakumbwa na mlipuko wa homa hiyo hatari ya mafua
makali muda mfupi ujao.
Homa ya mafua makali
(MERS) iliripotiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kutokea kwa mara ya kwanza
katika nchi ya Saudi Arabia mwaka mmoja uliopita, mpaka sasa idadi ya watu
walioripotiwa kuambukizwa Virusi vya mafua makali imefikia 94 huku watu 46 kati
ya hao wameripotiwa kupoteza maisha yao.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment