Watafiti kutoka chuo
kikuu cha Southampton, Britain wamegungua njia mpya ya kuwagundua haraka (screening)
watu wenye maambukizi ya TB (Tuberculosis) ili kuwapatia tiba na kuepusha
maambukizi yasiendelee kwa watu wengine. Njia iliyogunduliwa ni kutathimini
ongezeko la protini zinazotolewa na mapafu baada ya kuathirika.
Watafiti hao wamezitaja
protini hizo kuwa ni Collagen na Elastin ambazo ndizo protini kuu zinazopatikana
kwenye mapafu na kusema kwamba mtu anapoambukizwa TB protini hizo huongezeka kwenye
damu na kwenye makohozi hivyo iwapo sampuri ya damu au makohozi
itakapochukuliwa itaonyesha ongezeko hilo na kusaidia sana katika shughuli za
kuwatambua walioathirika na TB (screening), maendeleo ya kiuchunguzi na tiba
dhidi ya TB.
“hii itasaidia kwenye
uchunguzi wa watu wengi (screening) ili kuwapata na kuwatibia wale
walioathiriwa zaidi na kukata cheni ya maambukizi mapya, hii itasaidia sana mataifa
yanayoendelea ambapo ugonjwa wa TB umekuwa ni tatizo”. Alisema kiongozi wa
utafiti huo Bw. Paul Elkington.
Bakteria wa TB huathiri
Mapafu kwa kiasi kikubwa na kusababisha maambukizi kwa watu wengine kwa njia ya
hewa, iwapo mgonjwa hata pata matibabu kwa wakati anaweza kupoteza Maisha. Kwa mujibu
wa WHO, Zaidi ya vifo milioni moja na nusu vinavyosababishwa na TB hutokea kila
mwaka.
Matokeo ya utafiti huu
yamechapishwa kwenye Jarida la TheJournal of Infectious Diseases.
No comments:
Post a Comment