WATAFITI WAMESHAURI KIPAUMBELE CHA KUDHIBITI UGONJWA WA MALARIA KIWE KWENYE MAZALIA YA MBU




Ripoti ya utafiti wa kudhibiti ugonjwa wa malaria uliofanywa na watafiti kutoka  London School of Hygiene and Tropical Medicine, imesema kwamba kuweka kipaumbele kwenye kudhibiti mazalia ya mbu itasaidia sana kupunguza magonjwa ya malaria katika bara la Afrika na Asia.

Watafiti hao wakiongea na vyombo vya habari wamesema kwamba kwasasa mbu wamekuwa wakipingana kwa kiasi kikubwa na sumu za kuulia wadudu na hivyo mbinu mpya zinahitajika kuzibiti ugonjwa wa malaria.


Wamezitaja mbinu hizo kuwa ni pamoja na kuondoa madimbwi ya maji yaliyotuama sehemu ambayo lava wa  mbu hukulia na pia kutibu maji hayo kwa kemikali za kuulia lava wa mbu.

Zaidi ya watu 600,000 walikufa kwa  malaria mwaka 2010, idadi kubwa ya watu waliokufa walikuwa ni watoto wa Afrika.

Kwa muda wa muongo mmoja uliopita, idadi ya vifo vinavyotokana na malaria vimeshuka kwa ¼, mbinu kubwa iliyosaidia kushuka kwa vifo hivyo ni kusambazwa kwa vyandarua vyenye dawa ya kuuwa mbu ya muda mrefu (insecticides treated nets) na matumizi ya sumu za kuulia wadudu zinazopulizwa ndani ya nyumba (indoor insecticides sprays).

Pamoja na kushuka kwa hifo hivyo lakini watafiti hao wamesema mbu wamekuwa wakionyesha upinzani mkubwa kwa sumu za kuulia wadudu (insecticides) kwa kadiri muda unavyozidi kwenda na hivyo mamlaka husika zinatakiwa kutumia mbinu mpya inayojulikana kama “udhibiti wa lava wa mbu kwenye vyanzo vya mazalia”.

 Mbinu hii ni ile ambayo lava wa mbu anayepatikana kwenye maji yaliyotuama kama vile kwenye mashamba ya mpunga (paddy fields) au madimbwi, huuliwa kwa kutiririsha maji hayo na kulikausha eneo kabla lava hao hawajapata muda wa kukua. Pia mbinu hii hujumuisha kuuwa lava wa mbu kwa kumimina kemikali maalumu kwenye maji yaliyosimama.

Watafiti hao wamethibitisha kwamba mbinu hii iwapo itatumiwa vizuri inaweza kupunguza magonjwa ya malaria kwa asilimia 75 na kupunguza idadi ya watu walioambukizwa vimelea vya malaria kwa asilimia 90.


source: BBC


1 comment:

  1. Dr Parthasarthi has 18 years of rich experience in the field of Dermatology, Cosmetology and Trichology.
    best skin doctor in bangalore

    ReplyDelete