Na Goodluck Mselle (BSc. EHS)
Kuna watu ambao katika maisha yao
ya kila siku hawana tabia ya kunywa maji mara kwa mara . Hii ni kutokana na
kuona kero kwa kunywa maji kila wakati au kuona uvivu wa kubeba chupa za maji
au kulazimika kufuata mahali ambapo maji yanapatikana lakini kubwa kuliko zote
kati ya sababu hizo ni kutofahamu umuhimu wa kunywa maji mara kwa mara katika
maisha ya afya ya mwanadamu.
Maji ni sehemu muhimu ya maisha ya mwanadamu na yana
machango mkubwa sana katika afya ya mwili na kama yakinywewa ipasavyo yanaweza
kukuepusha na magonjwa mengi ambayo yatakufanya uishi maisha marefu .
Maji
yanakufanya uendelee kuonekana mdogo
Maji yanafanya ngozi yako iwe na vimeleo au mabaki
muhimu ya maji muda wote na hivyo kuondoa adha ya ngozi kuharibika kutokana na
umri mkubwa . Maji kiasilia hurutubisha ngozi huku ikijazia mistari ambayo
huondoa makunyanzi na kuifanya ionekana kuwa nyororo na laini.
Unywaji
wa maji huondoa Msongo wa mawazo
Unaweza ukashindwa kuamini jinsi gani maji yana
mchango kwenye afya ya saikolojia yako lakini ile sauti ya maji yakiwa
yanachuruzika inaweza kutuliza mawazo yako na kuondoa msongo wa mawazo .
Maji
yasaidia kupunguza na kuponya mafua
Unywaji wa maji husaidia kuondoa mafua kwa wale
wenye allergy ya vumbi na uchafu na pia kunawa mikono mara kwa mara kwa maji
masafi kunasaidia kuua vijidudu ambavyo huwafanya watu kupata mafua mara kwa
mara .
Maji yasaidia nywele
Kwa wale wadau wa masuala ya urembo hasa kina dada
zaidi ya kuritubisha ngozi maji husaidia kung’arisha nywele . Kuosha nywele kwa
maji ambayo hayajachemshwa kwa kutumia virutubisho vya nywele vya kutengeneza
kama vile shampoo na mafuta maalum aina ya conditioner yanazifanya nywele kuwa
thabiti zaidi na kuondoa uwezekano wa kungoka hovyo hovyo huku zikiwa na mn’gao.
Ngozi
ya mwili husaidiwa sana na maji
Zaidi ya ngozi ya uso maji ni muhimu kwa ngozi ya
mwili kwa ujumla . Wakati wa kuoga maji ya moto au vugu vugu hufanya ngozi ya
mwili kuwa nyororo na yenye afya zaidi , maji husaidia kuondoa ukavu ambao
huondoa mvuto wa asili wa ngozi na kuipa afya kwa ujumla.
Maji
husaidia kupunguza uzito wa mwili
Kwa wale wenye matatizo ya uzito ambayo wakati
mwingine yanaweza yakawa hatari kwa afya yako kwa kusababisha matatizo kama
Presha, kisukari na magonjwa ya moyo maji yanaweza kuwa kimbilio lako. Kwa
kujibu wa utafiti , watu wazima wanaokunywa glasi nane za maji kwa siku yaani
angalau glass mbili kwa kila baada ya saa kadhaa hasa kabla ya wakati wa kula
wanajikuta wakila chakula kidogo na hivyo kufanya mwili wako kupata chakula
kile kile kinachohitajika na mwili wako na hivyo kuondoa uwezekano wa mwili
wako kulimbikiza chakula kinachofanya uzito wako uendelee.
Maji
huisaidia akili kufanya kazi vizuri
Mwili unapokosa maji tatizo pekee sio mtu kuhisi
kiu wakati mwingine ubongo huhisi
kuchoka kirahisi na haraka pale ambapo mtu hajanywa maji muda mrefu . Hisia
kama hasira , uchovu wa akili , kuchanganyikiwa humtokea mtu kirahisi wakati
akiwa hajanywa maji muda mrefu na wakati mwingine hata kichwa huuuma sana
lakini suluhisho la yote haya ni kunywa maji mara kwa mara .
Muwasho
wa koo
Muwasho wa koo unaotokana na allergy au mafua
hutibiwa na maji , mtu anapopata tatizo hili suluhisho la haraka ni kusukutua
maji yenye chumvi lakini kuepsuah tatizo hili ni kuhakikisha koo halikauki kwa
muda mrefu.
Maji
husaidia kupigana dhidi ya magonjwa
Maji yana msaada mkubwa sana kwenye kupambana na
magonjwa mwilini mwako . Ni vizuri kunywa maji mara kwa mara kuepusha mwili
wako na magonjwa . Pia ulaji wa matunda husaidia kuupa mwili maji muhimu
yanayokuwa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali . Matunda kama mapapai,matikiti
maji,matango,machungwa ,ndizi,maembe yanauongezea mwili maji ambayo yanakufanya
ukae muda mrefu bila kuugua .
KDC Dental Academy is working hard to enhance the quality of continuing Dental Education.
ReplyDeleteImplant courses