FAHAMU KUHUSU UGONJWA HATARI WA EBOLA





Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kwa lugha ya kitaalam “Ebola Virus”. Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za Virusi zinaazosababisha kutokwa Damu mwilini, (Viral Haemorrhagic Fevers). 

Mnamo mwezi wa Machi 2014 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu ugonjwa wa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi ambao ulianzia katika ya nchi ya Guinea na kusambaa katika nchi za Siera Leone, Liberia na Nigeria. Mpaka kufikia Octoba, 2014 idadi ya vifo vilivyotokana na  ugonjwa wa Ebola imefikia watu 4,500.

 
(Maeneo yaliyowahi kukumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola)


Kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hadi sasa hapa nchini Tanzania hakuna mgonjwa yoyote aliyethibitishwa kuwa na virusi vya Ebola.


DALILI ZA EBOLA

Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa ni kati ya siku 2 hadi 21 baada ya kupata maambukizi. 
Dalili za ugonjwa huu ni:-
  •  Homa kali, inayoambatana na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili kama pua, njia ya haja kubwa na ndogo, mdomoni, masikioni, machoni n.k.
  • Kutapika damu 
  • Kuharisha damu
  •  Fizi kuvuja damu 
  • Kutokwa na damu na kuvia chini ya ngozi. Kwa sababu ya kutokwa na damu sehemu za haja kubwa na ndogo, choo na mkojo pia vitaonekana kuwa na damu.
NJIA ZA MAAMBUKIZI
Ugonjwa huu unaenea kwa urahisi sana na haraka kutoka mtu mmoja hadi mtu mwingine  kupita njia mbalimbali. 
Njia hizo ni:-  
  • kugusana na:- Mate,Damu, Mkojo, Machozi, Kamasi, Maji maji mengine ya mwili ikiwa ni pamoja na jasho.  
  • Kugusa mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa Ebola 
  • Kushika/kugusana au kula wanyama jamii ya nyani wenye virusi vya Ebola
  •  
  •                
  • Kuchomwa na sindano au vifaa ambavyo havikutakaswa 
  • Ugonjwa huu pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye virusi vya Ebola 
  • Kugusa taka ngumu au maji taka yaliyotokana na kumhudumia mgonjwa Ebola.

ATHARI ZA EBOLA
  •  Unasambaa kwa haraka sana. 
  • Unasababisha vifo vingi kwa muda mfupi 
  • Jamii huingiwa na hofu na wasiwasi na kushindwa kufanya shughuli zao za kawaida. 
  • Ni gharama kuwahudumia/kutibu wagonjwa. 
  • Mipaka inaweza kufungwa na watu wakashindwa kusafiri kutoka eneo/nchi moja hadi nyingine.

KINGA YA EBOLA

Ugonjwa wa Ebola hauna tiba wala chanjo bali unaweza kuzuilika. Njia kuu za kujikinga na ugonjwa huu ni:- 
  • Kuepuka kugusa au kuingiwa na mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na majimaji mengine yanayotoka mwilini mwa mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola. 
  • Kwa kuwa ugonjwa huu pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, epuka kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja 
  • Toa taarifa mapema kwa viongozi wa Serikali na wa huduma za Afya katika ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye dalili za Ebola. 
  • Jamii inahamashishwa kuwahi katika vituo vya huduma za Afya pale mtu anapoona dalili za ugonjwa huu. 
  • Wananchi wanatahadharishwa kuepuka kushughulikia maiti ya mtu aliyekufa akiwa na dalili za Ebola; badala yake watoe taarifa kwa uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa ushauri. 
  •  
  •                      
  • Wananchi waepuke mila na desturi zinazoweza kuchelewesha kupata huduma muhimu na kuzidi kueneza ugonjwa wa Ebola. 

----------KINGA NI BORA KULIKO TIBA, CHUKUA TAHADHARI-----------


1 comment:

  1. Nishida elimu inatakiwa izidi kutolewa na kudhibiti mipaka yetu. Its time for public health education

    ReplyDelete