SUMU ZA KUULIA WADUDU MASHAMBANI ZISIZOKIDHI VIWANGO (OBSOLETE PESTCIDES) ZAENDELEA KUWA TATIZO NCHINI




Shirika la kilimo na chakula duniani (FAO) limekisia kwamba nusu ya tani milioni moja za Sumu za kuulia wadudu zisizofaa (obsolete pesticide), zinazagaa maeneo yote ya nchi zinazoendelea.

Sumu hizi zenye kemikali za hatari, mara nyingi zimekuwa zikihifadhiwa kwenye vyombo vilivyoharibika ambavyo huruhusu kupenya kwa sumu kwenye ardhi na maji, hivyo kusababisha matatizo makubwa ya kiafya na kimazingira. Tanzania ni moja ya nchi zilizoathirika sana na matatizo hayo na kwa mujibu wa hesabu zilizofanywa mwaka 2008, zilibaini kuwepo kwa kilogramu 1,500,000 za shehena ya sumu za kuulia wadudu zisizofaa zikisubiliwa kuingia sokoni.

Hesabu za mwanzo zilizofanywa kati ya mwaka 1997 na 2000 ziligundua uwepo wa shehena tani 1,000 ya Sumu za kuulia wadudu zisizofaa katika sehemu 350 na tani 200 za uchafu wa tiba za wanyama (veterinary waste).



Akizungumza na Daily news juzi, mwenyekiti wa programu ya kusimamia shehena za Sumu za kuulia mwadudu Afrika (Africa Stockpiles Programme or ASP) Dr. Vera Ngowi amesema Sumu za kuulia wadudu zisizofaa (obsolete pesticide) ni zile ambazo hazipaswi kutumiwa tena kwa lengo lililokusudiwa au lengo lolote lile isipokuwa kuteketezwa katika njia zinazofaa (proper disposal).

Ameongeza kwamba sababu kuu zinazochangia kurundikana kwa Sumu za kuulia wadudu zisizofaa nchini ni mifumo mibovu ya ununuzi inayopelekea kununua shehena kubwa ambayo haikufuata mahitaji/matakwa ya wakulima, manunuzi yasiyoendana na muda wa mahitaji, ukubwa wa shehena usioendana na mahitaji sahihi ya wakulima, nembo zisizokidhi viwango, upungufu wa vitendea kazi bora, upungufu wa maghala na usimamizi hafifu wa shehena ghalani, kupokea misaada ya sumu hizo zaidi ya mahitaji, ukosefu wa ushirikiano kwa mawakala waagizaji, kutotumika kwa sumu hizo baada ya kupigwa marufuku kwa sababu za kiafya na kimazingira na hivyo huachwa zikiharibika kadiri muda unavyokwenda.

Dr. Vera Ngowi amesema kwamba watu hawawezi kufanikiwa kimaendeleo iwapo watakuwa wanaugua magonjwa yanayosababishwa na sumu za kuulia wadudu zisizofaa, magonjwa hayo ni pamoja na Saratani, Matatizo ya figo kushindwa kufanya kazi yake, na ugumba. Hivyo mamlaka husika zinapaswa kuwa makini kuzisoma sababu zinazopelekea kuzagaa kwa sumu za kuulia wadudu zisizofaa, wakulima pia wanatakiwa kupewa elimu juu ya matumizi na utunzaji sahihi wa sumu hizo ili kuondokana na madhara yake kiafya na kimazingira.


Kujua zaidi soma HAPA



No comments:

Post a Comment