FAHAMU ATHARI ZA KELELE KWENYE MAZINGIRA YA KAZI


Kufanya kazi mazingira ya kelele kunaweza kusababisha matatizo ya kiafya na kiusalama kwa wafanyakazi, tatizo linalojulikana kwa wengi ni kupoteza uwezo wa kusikia (hearing loss), japo yapo matatizo mengine zaidi yanayotokana na mazingira ya kelele. Ukurasa huu utakudadafulia matatizo mengine kwa kifupi ambayo ni vyema ukayajua ili kuchukua hatua katika eneo lako la kazi.

1.         Kuathirika kwa mfumo wa kusikia

Hii inaweza kusababishwa na kelele kubwa inayopelekea kuziba (mechanical blockage) kwa njia ya kusafirisha mawimbi ya sauti kwenda sehemu ya tatu ndani ya sikio au kuharibika kwa hair cell ndani ya cochlea ambayo ipo sehemu ya tatu ndani ya sikio. Tatizo hili linaweza kusababishwa na kufanya kazi katika mazingira ya kelele kwa muda mrefu, dalili ya kwanza ya tatizo hili ni kutosikia sauti zenye mawimbi ya kasi (high-pitched sounds) na iwapo tatizo la kelele halitashughulikiwa mapema basi hali itakuwa mbaya zaidi kwa kutosikia sauti za mawimbi ya taratibu (low pitched sounds).

2.         Tinnitus

Hii ni hali ambayo hujitokeza kwa mfanyakazi aliefanya kazi katika mazingira ya kelele kwa muda marefu, katika hali hii mfanyakazi huwa anajisikia milio na sauti zisizoeleweka anapokuwa katika eneo tulivu lisilokuwa na kelele, kelele za juu sana (mfano bundiki na mlipuko wa baruti) zinaweza kusababisha tatizo hili.

3.         Kuathirika kwa mtoto aliyeko tumboni

Tafiti zinaonesha kwamba mwanamke mjamzito anaefanya kazi katika mazingira ya kelele kuna uwezekano mkubwa wa kuathiri mfumo wa usikiaji wa mtoto aliyeko tumboni na hivyo kuzaa mtoto akiwa ana matatizo ya kusikia.

4.         Ajali makazini

Kelele kubwa katika mazingira ya kazi inaweza kuharibu mawasiliano baina ya wafanyakazi hivyo kushindwa kusikia milio ya dharura inayoashiria hatari (mfano: honi ya gari, milio ya hatari ya moto n.k), hali inayoweza kupelekea kupoteza maisha kutokana na ajali.


5.      Msongo wa mawazo (stress)

Kelele kubwa eneo la kazi husababisha matatizo kama maumivu kichwa, kupoteza utulivu (annoyance) na kukosa usingizi, matatizo haya kwa muda mrefu huwa yanazaa msongo wa mawazo (stress). Iwapo tatizo la msongo wa mawazo halitashughulikiwa mapema linaweza kupelekea ukichaa na matatizo mengine ya akili (mental disorders)


JINSI YA KUKABILIANA NA KELELE KWENYE MAZINGIRA YA KAZI

Kuna njia kuu tatu za kukabiliana na kelele katika eneo la kazi:

1.      `NJIA ZA KIINJIA

  •   Mainjia wanapaswa kubuni mashine zisizotoa kelele kubwa itakayosababisha athari za kiafya.
  •   Vyanzo vya kelele (mashine) vinatakiwa vifungwe mbali na maeneo ya kazi
  •  Vyanzo vinavyotoa kelele kutokana na uchakavu vinapaswa kubadilishwa au kurekebishwa ili kupunguza ukubwa wa kelele.
  •  Kama utenganishaji wa vyanzo vya kelele na maeneo ya kazi utashindikani basi inapaswa vifungwe vifaa maarumu vya kuzuia kelele (sound proof/mashine coverings)


2.      NJIA ZA KIUTAWALA
  • Utawala unapaswa kuwaepusha wafanyakazi kufanya kazi katika mazingira ya kelele kwa muda mrefu. Kulingana na sheria ya Afya na Usalama mahala pa kazi (OSHA), Manyakazi anaruhusiwa kufanya kazi kwenye mazingira ya kelele isiyozidi decibel 90 kwa muda usiozidi masaa 8.
  • Utawala unapaswa kuwaelimisha wafanyakazi juu ya madhara ya kelele maeneo ya kazi ili wawe na uelewa wa kujikinga na kelele.
  • Utawala unapaswa kutenga maeneo ya kazi yawe mbali na vyanzo vya kelele


3.   NJIA YA UTUMIAJI WA VIFAA KINGA

  •      Iwapo juhudi za kiinjinia za kupunguza kelele katika mazingira ya kazi zimeshindikana basi inashauliwa utawala uwapatie wafanyakazi vifaa kinga (protective equipments) kwa mfano plug na muffle za masikioni, na elimu ya jinsi ya kuvitumia vifaa hivyo kwa usahihi ili kujikinga na athari za kelele kiafya.


USALAMA KAZINI NI JAMBO LA MUHIMU SANA, JITATHMINI!!!!






No comments:

Post a Comment