(Imerekebishwa na kuchapishwa kutoka Gazeti la mwananchi, makala za Afya la tarehe 05/07/2013)
Dawa hizi zimekuwa zikitumika
katika nchi mbalimbali kwa sasa ikiwemo Tanzania, licha ya kuaminiwa na kuchukuliwa kama tiba bora zaidi
nchini, imegunduliwa kuwa dawa za mitishamba za Kichina zina chemchembe za dawa
za kuulia wadudu (kwa kitaalamu hujulikana kama pesticide).
Uchunguzi uliofanywa kupitia dawa hizo
zilizonunuliwa katika maduka mbalimbali yanayouza dawa hizo nchini Uingereza
umebaini kuwa dawa hizo zina kemikali zenye sumu zinazotokana na dawa za kuulia
wadudu.
Pamoja na ukweli kuwa kemikali
hizo zipo kwa kiasi kidogo sana , inasemekana matumizi ya dawa hizo kwa muda
mrefu yanasababisha uharibifu katika Vichocheo (hormone), matatizo katika mfumo
wa uzazi kwa wanaume na uharibifu wa mimba (reproductive disorder). Saratani (cancer)
na ulemavu wa akili.
Zaidi ya Waingereza milioni tatu
hutumia dawa za Kichina kujitibu kwa maradhi mbalimbali kila mwaka (sina idadi
kamili ya watumiaji wa Tanzania)
Katika kipindi cha miezi sita kuanzia
Novemba 2012 hadi Aprili 2013, wachunguzi wa Greenpeace walinunua
aina saba tofauti za dawa za mitishamba zilizoingizwa kutoka China kwa
ajili ya kuzifanyia majaribio.
Dawa hizo zilinunuliwa kutoka kwa
wauzaji wa rejareja kutoka kwenye nchi saba tofauti ikiwamo Uingereza. Dawa
hizo ni miongoni mwa zile zinazoaminiwa zaidi na wauzaji hao na pia zinadaiwa
kuwa tiba halisi ya magonjwa sugu ambayo yamekuwa wakiwasumbua watu wengi
hususan katika jamii ya Waasia.
Sampuli 26 kati ya 29
zilizochukuliwa kutoka Uingereza na maduka mengine barani Ulaya ziligundulika
kuwa kuna chembechembe za dawa za kuulia wadudu.Sampuli moja ya
‘honeysuckle’peke yake ilinunuliwa nchini Uingereza ilikuwa na viashiria 17 vya
dawa hiyo ya kuulia wadudu (pesticide), inayozidi nane katika kiwango cha
usalama cha Ulaya.
Akitoa maoni yake kuhusiana na utafiti
huo, mwanasayansi mkuu wa Taasisi Greenpeace ya Uingereza, Dk Doug Parr, alisema‘Sumu
zilizoko kwenye dawa hizi za kichina zinahatarisha afya za watumiaji wa dawa
hizo”
Kati ya bidhaa 36, zilizonunuliwa 32
kati yake zilikuwa zina chembechembe aina tatu za dawa hizo za kuulia
wadudu,17 kati yake zina chembechembe za dawa za kuulia wadudu zilizoanishwa na
shirika la Afya duniani (WHO).
Msemaji wa wakala wa udhibiti wa dawa na
afya wa Uingereza alisema ‘kuna baadhi ya dawa za kichina nchini Uingereza
ambazo pengine zimetengenezwa katika viwango vidogo vya ubora au kwa bahati
mbaya zimeingiziwa sumu ama viungo haramu.
Dk Kaicun Zhao, rais wa chama
cha dawa za asili za kichina nchini Uingereza alisema, “Tungesoma hili
kwa kina, pamoja na kufikiria kuwa inawezekana hii haihusishi dawa zote
zinazoingia kutoka China ndani ya soko la Uingereza na Ulaya kwa ujumla, kitu
muhimu tunachokiona hapa ni kusimamia viwango vya ubora vya dawa hizi, ni
matumaini yetu kuwa Uingereza na Ulaya kwa ujumla wataharakisha kuanzisha
utaratibu sahihi wa upimaji wa viwango vya ubora katika dawa za mitishamba
hususani dawa za Kichina”.
Je serikali yetu ya Tanzania kupitia
mamlaka ya dawa, chakula na vipodozi (TFDA) imejiandaa vya kutosha kukabiliana
na changamoto za uchakachuaji wa dawa za asili kutoka mataifa yenye teknolojia ya
juu kama China na India?????
No comments:
Post a Comment