Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira),
Dk.Terezya Huvisa, ametangaza kuyafunga machinjio ya Ukonga Mazizini yaliyopo
Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kutokana na kuendesha shughuli zake
katika mazingira machafu yanayohatarisha afya za walaji wa nyama.
Hii ni mara ya pili kwa machinjio hayo kufungwa na mamlaka za
serikali katika kipindi cha mwaka huu, mara ya kwanza Baraza la Taifa la
Usimamizi wa Mazingira (Nemc), liliyafunga kwa sababu kama hizo lakini siku nne
baadaye yaliendelea na shughuli zake kama kawaida.
Hatua ya machinjio hayo kuruhusiwa kuendelea na uchinjaji
siku chache tu baada ya kufungwa na Nemc kulizua maswali mengi kwa wananchi wa
kata ya Ukonga ambao walilitupia lawama baraza hilo kwamba huenda baadhi ya
maofisa wake walipewa ‘kitu kidogo’ na kulegeza masharti.
Akizungumza na wananchi wa Ukonga Juzi majira ya saa 3:30 asubuhi baada
ya kufanya ziara ya kushtukiza katika machinjio hayo, Waziri Huviza alisema
anayafunga kutokana na kuendesha shughuli zake katika mazingira machafu.
Alisema sababu nyingine ni kwamba machinjio hayo ambayo yameanza kuendesha shughuli zake tangu mwaka 1972, katika kipindi chote yamekuwa yakiendesha kazi zake bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Nemc kama sheria zinavyoelekeza. Waziri Huvisa aliwaagiza maofisa wa Nemc, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mazingira wa baraza hilo, Robert Mtakamalenga, kuandika barua haraka ya kusimamisha shughuli za uchinjaji katika machinjio hayo na kuiwasilisha kwa wamiliki wake jana.
Alisema athari ambazo zitakuwa zimepatikana kwa wananchi kutokana na miundombinu mibovu ya mifereji ya kupitishia maji machafu uliopita karibu na makazi ya watu wamiliki wa machinjio hayo watawajibika kulipa gharama kwa waathirika.
Akisoma taarifa kwa niaba ya wananchi wa kata ya Ukonga wanaoathirika kutokana na uchafu wa machinjio hayo, Bennett Bagonza, alisema hawana imani Nemc na Manispaa ya Ilala ambayo viongozi wake kila wanapoelezwa suala la uchafu katika machinjio hayo wamekuwa wakipuzia.

Chanzo: BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment