Utafiti uliofanywa na
Dk. Mandy Belfort akishirikiana na
wataalamu wengine kutoka Hospitali ya watoto ya Boston, Marekani, umegundua
kwamba wamanawake walionyonyesha watoto wao mwezi mmoja zaidi ya muda ulioshauriwa
na wataalamu wa afya (miezi sita bila kula chakula cha aina yoyote), watoto wao
wamekuwa wakifanya vizuri kimasomo ukilinganisha na watoto wengine.
Dk. Belfort amesema matokeo
ya utafiti huo yanalingana na ushauri ambao umekuwa ukitolewa kwa wanawake
wanaonyonyesha kwamba wahakikishe wanamnyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee mpaka
afikishe umri wa miezi sita ndipo waanze kunchanganyia maziwa ya mama na
vyakula vingine vigumugumu.
Utafiti huo ulifanyika
kwa kuwafuatilia wanawake wa mji wa Massachusetts pindi walipokuwa wajawazito
mnamo mwaka 1999 hadi 2002 na watoto wao.
Akina mama waliulizwa
kama wamewahi kuwanyonyesha watoto wao, na kama waliwanyonyesha, basi waliwaachisha
watoto wao wakiwa na umri gani. Baada maswali hayo watafiti waliwapa mtihani wa
kupima uwezo wa akili (intelligence) akina mama na watoto wao.
Watoto wa miaka mitatu
walipewa mtihani wa lugha, watoto hao walipata wastani wa alama 103.7. uwezo wa mama kiakili na mambo mengine ya
kijamii ikiwemo kipato vilitazamwa kwenye utafiti huu. Baada ya zoezi hilo
watafiti waligundua kwamba kila mtoto aliyenyonyeshwa mwezi mmoja zaidi ya ile
iliyoshauriwa (miezi sita) alipata pointi 0.21 zaidi ya wale walionyonyeshwa
miezi sita kamili.
Watoto walionyonyeshwa
maziwa ya mama pekee kwa muda wa miezi sita kamili tangu wazaliwe walipata
wastani wa pointi 3 zaidi ya wale ambao hawajawahi kunyonyeshwa maziwa ya mama.
Watoto wenye umri wa
miaka saba walipewa mtihani wa kusoma na kuandika, watoto wote walipata wastani
wa alama 112.5 huku kila mtoto aliyenyonyeshwa maziwa ya mama mwezi mmoja zaidi
ya muda ulioshauriwa (miezi sita) walipata point 0.35 zaidi ya wale
walionyonyeshwa maziwa ya mama kwa miezi sita kamili.
Kujua zaidi bofya HAPA
No comments:
Post a Comment