Imedondoshwa kutoka Gazeti la Mwananchi
Ni wengi wanaoutumia na kuufahamu
mchaichai kama kiungo cha chakula jikoni na wengine hutumia kama dawa ya
mbu.
Lakini, je unafahamu kuwa majani haya
yana faida kubwa kiafya . Mafuta ya mchachai hutumika katika viwanda
vinavyotengeneza pafyumu na sabuni.
Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa mchaichai
una vichocheo muhimu vinavyoweza kupambana na athari kadha wa kadha
tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda. Watu wengine huamini kuwa
mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile homa ya matumbo, matatizo
ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia
hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli.
Mchaichai pia unatajwa kuwa kinywaji
kinachoweza kupunguza joto. Chai ya mchaichai inasaidia kupunguza joto kwa
mgonjwa wa homa. Faida nyingine za mchaichai kiafya ni pamoja na:
Kinga
dhidi ya saratani
Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa
kwenye kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha sumu ambavyo vina uwezo wa
kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani. Mwaka 2006, timu ya watafiti
kutoka Chuo kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai una uwezo wa
kuua seli zinaweza kusababisha saratani.
Husaidia
umeng’enyaji wa chakula
Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu
wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo
ikiwamo kujaa gesi.
Hurahisisha utaratibu wa
kuondoa uchafu mwilini.
No comments:
Post a Comment