“Usipokula Matunda na
Mbogamboga unakufa mapema”. Hii ndio ilikuwa hitimisho ya utafiti uliofanywa nchini sweeden na
kuchapishwa hivi karibuni katika jarida
la Clinical nutrition la Marekani unaoonesha kwamba watu wanaokula milo mitano
ya matunda na mbogamboga kwa siku, wanaishi maisha marefu zaidi ya wale
wanaokula chini ya milo mitano kwa siku au wasiokula kabisa.
Utafiti ulifanywa kwa kuwahusisha
wasweeden 71,000 wenye umri kati ya miaka 45 mpaka 83, ambapo milo yao
waliyokuwa wanakula ilichunguzwa kwa muda wa miaka 13. Wale waliokuwa wanakula
angalau mlo mmoja wa matunda kwa siku waliishi miezi 19 zaidi ya wale ambao
hawakula matunda matunda, na wale waliokula angalau milo mitatu ya matunda na
mbogamboga kwa siku, waliishi miezi 32 zaidi.
Watu ambao waliripotiwa
kwamba hawakuwahi kutumia matunda na mboga mboga walikufa miaka mitatu (3)
kabla ya wenzao.
Mpaka utafiti
ulipokamilika mnamo mwezi Desemba 2010, tayari watu 11,500 waliohusishwa kwenye
utafiti huo walikuwa wameshatangulia mbele za haki (wamekufa).
Utafiti huo pia
ulibaini kwamba wanawake hula matunda na mbogamboga kwa wingi kuliko wanaume, japo
haukuweka wazi iwapo kuna uhusiano wowote wa vifo na jinsia. Watafiti pia
walizingatia mambo mengine katka utafiti wao kama vile jinsia, uvutaji sigara, mazoezi ya
mwili, unywaji wa pombe, uzito wa mwili lakini mwisho wa siku hayakuweza
kubadili matokeo yao.
Kujua zaidi bofya HAPA
No comments:
Post a Comment