SAUDI ARABIA IMETOA TAHADHARI KWA MAHUJAJI JUU YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA MFUMO WA HEWA (CORONAVIRUS)


Maafisa wa Afya nchini Saudi Arabia wamewaomba Mahujaji wanaoenda kuhiji maeneo matakatifu, kuchukua tahadhari kwa kuvaa masks katika sehemu zote zenye mkusanyiko mkubwa wa watu ili kuepukana na maambukizi/usambazaji wa virusi (coronavirus) vinavyoeneza ugonjwa wa mfumo wa hewa unaojulikana kama MERS (Middle East Respiratory Syndrom).

Moja ya tahadhali zilizotolewa na wizara ya Afya ya Saudi Arabia ni kuwaomba wazee na watu wote wenye magonjwa sugu kuahirisha safari zao za kwenda kuhiji.

Mpaka sasa Virusi hivyo vimeshaua watu 38 nchini humo.

Mamilioni ya waislamu kutoka duniani kote wanategemewa kwenda Makka Saudi Arabia kuhiji na kutembelea maeneo mengine ya Ibada kama Masjid Al-Nabawi, na Msikiti wa Mtume huko Madina, mwezi wa October mwaka huu , safari hizi hufanyika mara moja kwa mwaka.

Maafisa wa Afya wamewataka watu wote inchini Saudi Arabia kufuata masharti ya kiafya ikiwa ni pamoja na kutumia tissue au vitambaa wakati wa kupiga chafya na kukohoa, na kupatiwa chanjo muhimu ya kujikinga na maambukizI.

virusi vya MERS (Middle East Respiratory Syndrome Coronavirus) vilizuka katika peninsula ya uarabuni (Arabian peninsula) mwezi septemba mwaka 2012, virusi hivi ni moja ya jamii kubwa ya virusi kati ya vile vienezavyo mafua na Sars (Severe acute respiratory syndrome).

Shirika la Afya duniani (WHO) limethibitisha kwamba jumla ya wagonjwa 80 duniani kote wameambukizwa virusi hivyo, na 44 kati ya hao tayari wamepoteza maisha.


Source: BBC news



No comments:

Post a Comment