Mlipuko wa ugonjwa wa
Polio ambao uligundulika kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya mwezi
Mei mwaka huu, umeripotiwa kusambaa kona zote za nchi ya Somalia.
Wizara ya Afya nchini
Somalia imethibitisha kuwepo kwa maambukizi mapya 94 ya ugonjwa wa Polio Kusini
na Kati ya Somalia na pia kumekuwa hakuna Dalili zozote za kupunguza maambukizi
mapya nchini humo.
Maambukizi mapya
yameripotiwa na Shirika la habari la VoA kutokea karibu na mpaka wa Ethiopia na kuifanya nchi hiyo na nchi
zinazopakana na Somalia ziwepo hatarini kupata maambukizi mapya ya ugonjwa huo.
Hapo mwanzo ugonjwa huu
ulikuwa umetokomezwa duniani kote kabla ya maambuzi mapya ambayo yameripotiwa
hivi karibuni kutokea kwenye nchi tatu: Afghanistani, Pakistan na Nigeria.
Polio ni ugonjwa
unaoambukizwa na kirusi ambacho hushambulia Mfumo wa fahamu (nervous system) na
kusababisha mtu kupooza misuli na kuwa Mlemavu wa viungo, iwapo kirusi kitashambulia misuli
ya kifua kinaweza kusababisha KIFO. Kirusi hiki husambazwa kutoka kwa mgonjwa
wa polio kwenda kwa mtu mwingine kupitia kinyesi cha mtu aliyeathirika.
Ugonjwa huu hauna tiba
bali hukingwa kwa Chanyo ya polio, hivyo inashauriwa watoto wote wanaozaliwa
wapate Chanjo ya kujikinga na ugonjwa huu hatari. Pia kila mtu anashauriwa
kujisaidia chuoni ili kuepusha kusambaa kwa vinyesi (MAVI) vilivyosheheni virusi
vya polio kwenye mazingira ambavyo vinaweza kuwa hatari kwa watoto wanaotambaa,
watu wanaokula udongo, watu wanaokunywa maji yanayotoka kwenye chanzo
kilichochafuliwa n.k.
No comments:
Post a Comment