UTAFITI: VINYWAJI VYA CHUPA ZA PLASTIKI VINAONGEZA HATARI YA KUPATA SARATANI KWENYE TUMBO LA UZAZI



Utafiti uliofanywa nchini Marekani umeonesha kwamba wanawake wajawazito wanaokunywa vinywaji vya chupa za plastiki wanaongeza hatari ya watoto wao watarajiwa kupata saratani kwenye maisha yao ya baadae.

Utafiti huo uliofanywa kwa panya wa maabara (mice) na watafiti wa Chuo kikuu cha Illinois, ulionesha kwamba chupa za plastiki zina kemikali hatari zinazojilikana kwa kitaalamu kama Bisphenol A (BPA) ambazo zikiingia kwenye tumbo la uzazi kupitia vinywaji vilivyopo ndani ya chupa hizo zitaongeza hatari ya kwa mtoto mtarajiwa kupata Saratani ya tezi za uzazi (prostate Cancer).  Imeripotiwa na shirika la habari la Daily.

Kiongozi wa utafiti huo, Gail Prins amesema zaidi ya asilimia 95 ya wamama watarajiwa nchini marekani wamekutwa na kemikali ya (BPA) kwenye matokeo ya vipimo vya mkojo hali inayoashiria kwamba wamekunjwa kemikali hii hatari kupitia vinjwaji vya chupa za plastiki.

Utafiti ulifanywa kwa Panya wa maabara (mice) kwa kuwapandikizia chembechembe za uumbaji wa tezi za uzazi (prostate stem cells) na baada ya wiki mbili Panya hao wakanyweshwa kiasi cha kemikali hatari ya BPA sawasawa (equivalent) na kile kilichokutwa kwa wamama wajawazito. Baada ya kunyweshwa BPA wakaongezewa kiasi cha vichocheo vya Oestrogen (oestrogen hormone) sawasawa (equivalent) na kiasi cha vichocheo hivyo vinavyopatikana kwa wanaume wanaokua.

Dalili za saratani zilianza kujitokeza kwenye tishu za tezi za uzazi (prostate tissue) za robo tatu ya panya walionyweshwa BPA ukilinganisha na asilimia 12 ya Panya ambao hawakunyweshwa kemikali hiyo.




Kusoma zaidi BOFYA AFYA 



No comments:

Post a Comment