UTAFITI: KUNA UHUSIANO MKUBWA KATI YA WATU KUKOSA USINGIZI NA MWEZI KAMILIFU (FULL MOON)



Watu wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu kukosa usingizi usiku hasa hasa kipindi ambapo mwezi unakuwa kamilifu (full moon), sasa utafiti mpya umepata uthibitisho kwamba mwezi unapokuwa karibu sana na sayari ya Galaxy huwa unatoa athari kwenye usingizi wa binadamu.

Christian Cajochen, mtafiti wa masuala ya usingizi kutoka Hospitali ya magonjwa ya Akili ya Chuo kikuu cha Basel, Switzerland, aliongoza utafiti wa kuchambua taarifa za vipimo vya usingizi (ikiwemo utendaji kazi wa ubongo) kwa watu 33 ambao walikuwa wakifanyiwa tathimini kwenye kliniki ya matatizo ya ukosefu wa usingizi usiku.

Cajochen alisema “katika kipindi cha mwezi kamilifu (full moon), watu huwa wanapata usingizi mnono (deep sleep) kwa muda mfupi wa kama asilimia 30 ya usingizi mnono wa kawaida, kwa ujumla huwa wanatumia dakika tano kupata usingizi na wakipata usingizi mnono huwa haudumu zaidi ya dakika 20”.

Cajochen alisema usingizi huwa unachochewa na mfumo wa masaa 24 uliozoeleka ndani ya mwili ambao kwa kitaalamu hujulikana kama Circadian rhythm, mfumo huu wa kibaiolojia huwa unaendeshwa na mabadiliko ya vichocheo (hormone fluctuations) ambayo huwa yanaendesha mzunguko wa kulala-kuamka na mpangilio wa kula chakula. Mabadiliko haya ya vichocheo pia huwa yanaathiriwa na uwepo wa mwanga na giza.

“miili yetu imekalili tabia za wakati wa usiku (giza) ikiwemo kulala, hivyo ifikapo usiku (giza) miili hutoa vichocheo vinavyotuandaa kulala (sleep-preparatory hormone), vichocheo hivyo kwa kitaalamu hujulikana kama Melatonini hormone. Vichocheo hivi huwa vinapungua sana kipindi cha mwezi kamilifu (kutokana na kuongezeka kwa mwanga wakati wa usiku)  na kupelekea mtu kukosa usingizi”. Cajochen alisema.



No comments:

Post a Comment