UTAFITI WA KUWEZA KUTIBU UPOFU WAANZA KUZAA MATUNDA



Utafiti unaofanywa na wanasayansi wa UK kuhusu tiba ya kuponya upofu (blindness) umeanza kuzaa matunda baada ya matokeo ya utafiti huo kwa panya kuonesha kwamba sehemu ya jicho ambayo hupokea mwanga (photoreceptors) inaweza kutibiwa (repared) kwa kutumia chembechembe za uumbaji (embroyonic steam cell).

Photoreceptors ni chemechembe (cells) zilizopo ndani ya retina ambazo hufanya kazi ya kupokea mwanga na kubadilisha mfumo wa mwanga kwenda kwenye mfumo wa umeme ambao hutumwa kwenye ubongo, na baada ya kupokea, ubongo unaweza kutafsiri picha iliyojitokeza kwenye mwanga.

Chembechembe hizo (photoreceptors) zinaweza kufa kutokana na magonjwa ya macho (mfano trakoma, stargardt) au kulegea kwa misuli ya macho inayotokana na uzee, na hivyo kupelekea mtu kuwa kipofu.

Utafiti huo ulifanywa kwa kutengeneza retina kwenye maabara ambapo maelfu ya chembechembe za uumbaji (embryonic stem cell) zilikusanywa na kupandikizwa kwenye eneo la photoreceptors zilizokufa, baada ya upandikizi huo retina hiyo ilichukuliwa na kuingizwa kwenye jicho la panya aliekuwa kipofu. Baada ya muda chembechembe hizo zilianza kujengeka kulingana na umbo la jicho na kuanza kufanya kazi, hali iliyompelekea panya kupona upofu na kuanza kuona upya.

Mtaalamu anaeongoza utafiti huo, Prof Robin Ali aliliambia shirika la habari la BBC kwamba “huu ni uthibitisho tosha wa dhana kwamba photoreceptors zinaweza kupandikizwa kutoka kwenye chembechembe za uumbaji (embryonic stem cells) hivyo utafiti huu unatupa picha mpya kwamba tunaweza kufanya  hivi hata kwa binadamu”.


Kusoma zaidi bofya HAPA




No comments:

Post a Comment