Utapiamlo kwa watoto ni
Moja ya Matatizo makubwa yanayoikabili Dunia kwa sasa, tatizo hili limezikumba nchi
nyingi sana Duniani hasa nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara (ikiwemo
Tanzania) na Asia ya kusini.
Utafiti wa hivi
karibuni uliochapishwa katika Jarida la Tiba la Lancet (Lancet medical jornal)
unaonesha kwamba utapiamlo husababisha Asilimia 45 ya vifo vyote vinavyotokea
kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Watoto wengine hudumaa kimwili
na Ubongo kushindwa kufanya kazi yake kama inavyotakiwa (Moja kati ya kazi ya
ubongo ni Kufikiria)
Dr. Robert Black wa
chuo kikuu cha Johns Hopkins ambae alihusika katika utafiti huo alisema kwamba Utapiamlo
unaweza kumkumba mtoto tangu akiwa tumboni iwapo mama mjamzito atakuwa hana
lishe bora (mwenye utapiamlo) hivyo hata kama mtoto atazaliwa, uwezekano kifo,
kudumaa kimwili na kiakili utakuwa ni mkubwa sana.
Utafiti huo unaonesha
kwamba kuwekeza kwenye lishe bora ya watoto kutaongeza ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kuongezeka kwa watoto
wanaofanya vizuri mashuleni na hatimae kuwa watu wenye uwezo mkubwa wa
kufikiria na nguvu kazi bora kwa Taifa.
Pia imebainika kwamba
mtu mzima aliewahi kuwa na utapiamlo utotoni anaingiza kipato cha asilimia 20
pungufu ya mtu Yule ambaye alikulia katika lishe bora.
Mtoto na mtu mzima
mwenye utapiamlo hukumbwa na maradhi mengi kwa kuwa kinga yake dhidi ya magonjwa
huwa inashuka hivyo wazazi na Taifa kwa ujumla hupoteza pesa na muda mwingi kutafuta
Tiba badala ya kufanya shughuli za uzalishaji uchumi hali inayopelekea kuongezeka kwa Umasikini,
hivyo ni vyema kwa wananchi na Serikali kuamka na kuanza kupalilia lishe bora
za watoto tangu wakiwa tumboni ili kuhakikisha tunatengeneza Taifa la watu
MAKINI.
No comments:
Post a Comment