BURGER YA KWANZA KUTENGENEZWA MAABARA



Ulimwengu hauishi maajabu, vituko na vijambo. je waweza kuamini kwamba burger ya kwanza kutengenezwa maabara kwa kutumia seli za ng’ombe imepikwa na kuliwa katika mkutano wa habari jijini London!?

Habari zilizoifikia ‘AFYA YA MAZINGIRA’ zinasema kwamba burger hii ilitengenezwa maabara kwa kutumia seli kutoka kwa mnyama aina ya Ng’ombe ambapo seli hizo zilioteshwa maabara hadi zikawa nyama (muscles) kisha nyama hiyo ikatumika kutengeneza chakula kinachopendwa na wengi aina ya burger.

Ubunifu huu wa kutengeneza nyama kwa kutumia seli za ng’ombe unakuja miezi michache tangu shirika la chakula na kilimo duniani (FAO) kutangaza kwamba baada ya miaka kadhaa watu watalazimika kula wadudu kutokana na uhaba wa chakula unaoelekea kuikumba dunia kutokana na ongezeko kubwa la watu (high population) na uhaba wa mvua unaotokana na mabadiliko ya hali ya hewa (climatic change).

Wanasayansi waliobuni teknolojia hiyo wanasema “teknolojia hii itasaidia sana kutokana na kuongezeka kwa watu wengi duniani wanaohitaji vyakula vinavyotokana na nyama”.

Mmoja wa watu waliofanikisha kuionja nyama hiyo ni mtafiti wa chakula wa Austraria, Bw. Ruetzler ambapo baada ya kuionja alisema “nilidhania kwamba nyama hii ingekuwa laini sana…ina radha nzuri inayofanana na nyama lakini haina majimaji kama nyama ya kawaida”.

 “Ufanano uko sahihi kabisa japo kuwa nimekosaa chumvi na pilipili”. Bw. Ruetzler alitania.

Akiongea na vyombo vya habari, kiongozi wa utafiti uliogundua teknolojia hiyo mpya, prof. Mark Post kutoka chuo kikuu cha Maastricht amesema nyama hiyo imetengenezwa kwa kutumia idadi ya mabilioni ya seli zilizo kuzwa maabara, na kuongeza kwamba itachukua muda kidogo hadi pale nyama hizo zitakapoanza kusambazwa masokoni.



1 comment:

  1. WE ARE FACING PROBLEM OF GETTING THESE
    IMPORTANT STUFFS ....WE NEED TO BE PUBLIC SO THAT MANY PEOPLE CAN GET THEM EASY .
    EVERYTHING THAT WE DO LET THEM BE ACESIBLE SO THAT EVERYBODY CAN GET WHAT WE ARE IMPORTANT TO A WHOLE SOCIETY .LET US BE COMMITED TO
    SAVE LIFE
    SERVE PEROPLE
    AND SERVE OURSELVES THEN

    ReplyDelete