MACHINJIO YA VINGUNGUTI DAR ES SALAAM YAVAMIWA



Ni wiki moja tu imepita tangu Serikali iifunge machinjio ya Ukonga Mazizini kutokana na kuendesha shughuli zake kwenye hali ya uchafu, mabucha yaliyokuwa Ukonga mazizini yamehamishiwa karibu na machinjio ya vingunguti na kupelekea hali ya mazingira ya uchafu maeneo hayo.

Msimamizi wa machinjio ya Vingunguti, Dk. Juma Nganyagi amethibitisha kutokea kwa hali hilo na kusema kwamba uongozi unalifanyia kazi suala hilo.

Machinjio ya Ukonga mazizini ilifungwa na waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa rais (mazingira), Dk. Terezya Huvisa kwa kuendesha shughuli zake katika mazingira ya uchafu na kuhatarisha Afya za walaji wa nyamba.

Uchunguzi uliofanywa na vyombo vya habari umeonesha kwamba watu wengi waliokuwa wanafanyia shughuli zao kwenye machinjio ya Ukonga Mazizini wamehamia machinjio ya Vingunguti na kuongeza idadi ya ng’ombe wanaochinjwa machinjioni hapo zaidi ya mara mbili. Kwasasa miundombinu ya machinjio hiyo imezidiwa na ongezeko kubwa la wanyama wanaochinjwa na wanaosubiri kuchinjwa.

Pia uchunguzi huo umebaini kwamba hali ya usafi na afya maeneo hayo imekuwa mbaya sana kwakuwa waendeshaji wa shughuli za uchinjaji machinjioni hapo hawafuati sheria za Afya na Mazingira.

Kusoma zaidi BOFYA HAPA



No comments:

Post a Comment