Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imetoa wito kwa
wananchi kutotumia chupa za kulisha watoto, maarufu kama ‘nyonyo au chuchu za
watoto’ kwa ajili ya kuwanyonyeshea watoto, kwa kuwa huwasababishia magonjwa na
hatimaye vifo.
Badala yake imewaasa watumie vikombe vilivyosafishwa kwa sabuni na majimoto kumlishia mtoto, ili akue akiwa na afya njema.
Wito huo umetolewa juzi jijini Dar es Salaam na Mtaalamu wa Unyonyeshaji Watoto wa TFNC, Neema Joshua, kwenye semina ya mafunzo maalumu kwa wanahabari, yaliyoendeshwa na TFNC kwa ajili ya wiki ya unyonyeshaji duniani.
Neema alisema, chupa nyingi zinazotumiwa nchini kwa lengo la kunyonyeshea watoto hazifai, kutokana na ugumu wa kuzisafisha.
“Nyingi ya chupa hizo ambazo zimesambaa karibu nchi nzima husababisha magonjwa kwa watoto, yakiwamo ya kuharisha kutokana na ugumu wa kuzisafisha. Na ndiyo maana tunaelekeza kikombe kilicho safi kitumike, badala ya chupa hizi,” alisema.
Akiongea kwenye uzinduzi wa Wiki ya Unyonyeshaji Duniani uliofanyika jana jijini Dar es salaam, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi alisisitiza umuhimu wa kulinda, kuboresha na kusaidia kuendeleza utamaduni wa unyonyeshaji watoto wa maziwa ya mama pekee.
Kupitia kwenye tamko lake lililosomwa mbele ya waandishi wa habari na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Donnan Mmbando, Dk. Mwinyi alisema kwamba unyonyeshaji watoto wa maziwa ya mama, hutoa mchango mkubwa wa kupunguza kasi ya maradhi na vifo vya watoto.
“Tunahimiza watoto wanyonye maziwa ya mama pekee kwa muda wa miezi sita ya mwanzo, bila ya kupewa maji, vinywaji au vyakula vingine…tafiti zinaonyesha kwamba hupunguza vifo vya watoto kwa asilimia 13,” alisema.
Kauli mbiu ya wiki ya unyonyeshaji duniani kwa mwaka huu, ni ‘Tumsaidie Mama Ili Aweze Kunyonyesha kwa Ufanisi Zaidi.

Source: NIPASHE
No comments:
Post a Comment