Matokeo ya utafiti
uliofanywa na Jopo la watafiti hapa nchini kwenye wilaya 12 za Tanzania na
kuchapishwa kwenye jarida la Tanzania Journal of Heath Research umeonesha
kwamba kuna baadhi ya maeneo hapa nchini ambayo mbu wake wanaweza kupingana na
nguvu za sumu za kuulia wadudu na hivyo kushusha uwezekano wa mbu hao kufa kwa
sumu hizo.
Utafiti huo yameonesha kwamba
aina ya mbu maarufu kwa kubeba vimelea vya maralia hapa Tanzania, Anopheles
gambiae huathiriwa kwa kiasi kikubwa na sumu aina ya permethrin, deltamethrin,
lambdacyhalothrin na DDT, maeneo mengi kwenye utafiti huu yalionesha uwezekano
wa mbu hawa kufa kwa sumu hizi ni asilimia 98-100%.
Pamoja na matokeo hayo,
kuna baadhi ya maeneo hapa Tanzania ambayo yalionesha upinzani kwa Sumu hizo za
kuulia wadudu na kushusha uwezekano wa kufa kwa mbu hao hadi kufikia asilimia 80-97;
mbu wa Ilala walionesha upinzani kwa sumu ya DDT na kushusha uwezekano wa kufa
kwa sumu hiyo hadi kufikia asilimia 65, mbu wa Moshi walionesha upinzani kwa
sumu ya lambdacyhalothrin na permethrin na kushushwa uwezekano wa kufa hadi
kufikia asilimia 73 kwa lambdacyhalothrin na asilimia 77 kwa permethrin.
“kila baada ya muda fulani
vipimo vinapaswa kuchukuliwa (monitoring) kwa maeneo yote nchini ili kubaini
uwezo wa mbu kuathiriwa (susceptibility status) na sumu kabla ya kuamua
kuzitumia”. Ilishauri moja ya sehemu ya utafiti huo.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment