WATU wanne wa familia moja wamefariki na
wengine 13 wamelazwa hospitalini kutokana na kula chakula chenye sumu wakati wa
sikukuu ya Idi el Fitri.Watu hao wamelazwa Kituo cha Afya cha Lusewa wilayani
Namtumbo na Hospitali ya Serikali ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO).
Kamanda wa Polisi Mkoa Deusidebit Nsimeki,
alisema tukio hilo lilitokea Agosti 9, mwaka huu saa 7:00. Kamanda Nsimeki,
alisema siku hiyo kabla ya tukio, Salum Mumba, alinunua samaki aliyepeleka
nyumbani kwa ajili ya sikukuu ya Idi.Kamanda Nsimeki alisema katika tukio hilo
polisi wanamshikilia mtu mmoja ambaye hakutaka kumtaja jina ambaye atasaidia
polisi kwenye upelelezi wake.
Alisema baada ya kula chakula hicho,
haikuchukua muda mrefu mtoto alianza kuumwa naye baadaye alifariki dunia.
Baadaye watoto wawili walianza kuumwa na kufariki. Watu wengine 13 walianza
kuumwa baadaye majirani walipata taarifa na kuwakimbiza watu hao hospitali.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment