Mkurugenzi wa NIAID, Antony Fauci
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazotarajiwa
kufanyiwa majaribio ya chanjo ya ugonjwa hatari wa Malaria, ambayo tayari
imeonyesha mafanikio makubwa, Wanasayansi wa Marekani wameeleza.
Hii ni baada ya wanasayansi nchini Marekani kugundua chanjo aina ya PfSPZ, ambayo mtu akipatiwa hataugua tena ugonjwa wa malaria maisha yake yote. Taarifa iliyochapishwa kwenye jarida la Sayansi Agosti 08, yenye jina: "Ulinzi dhidi ya Malaria na chanjo ya PfSPZ."
Jarida la Nature liliripoti kwamba majaribio hayo yatafanyika nchini katika Taasisi ya Afya Ifakara.
Taarifa ya Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (NIAID), iliyotolewa Alhamisi iliyopita ilieleza kuwa, ugunduzi huo ambao tayari umefanyiwa majaribio kwa watu zaidi ya 36, umeonyesha mafanikio kwa asilimia 100 na kwamba utaandika historia ya kufuta malaria na kuwa ugonjwa wa nadra kwa watu kuugua.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mtu akipatiwa chanjo hiyo mwili wake unatengeneza kinga ambazo zinakuwa na uwezo wa kuangamiza vimelea wa malaria katika hatua yake ya mwanzo mara baada ya kuumwa na mbu.
Matokeo ya uchunguzi huo yanaelezwa kuwa mazuri kuwahi kutokea katika chanjo zote za malaria zilizowahi kugunduliwa.
Kwa mujibu wa jarida la Nature, Mkurugenzi wa NIAID, Anthony Fauci, alisema matokeo hayo ni hatua kubwa baada ya utafiti wa miaka mingi; na kwamba sasa imebainika kwamba uwezekano wa mtu kutougua malaria upo.
Akizungumza na kituo cha CNN, alisema: “Tatizo la malaria duniani siyo la kawaida na halikubaliki … ugunduzi huu umetupa mafanikio makubwa.”
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 200 duniani huugua malaria na takribani watu 500,000 hadi milioni moja hufariki dunia hususani walio kwenye nchi zinazoendelea za kitropiki.
Ugunduzi huo umekuja wakati ambao WHO imejiwekea lengo la kupata chanjo ya malaria kwa asilimia 80 ifikapo mwaka 2025 hivyo chanjo hiyo yenye uwezo wa kuzuia malaria kwa asilimia 100 imevuka lengo la shirika hilo.
Wanasayansi hao wameeleza kwamba majaribio zaidi ya chanjo hiyo yatafanyika barani Afrika na hususani Tanzania.
Timu ya utafiti wa timu hiyo iliongozwa na Stephen Hoffman, ambaye ni mtaalamu wa utafiti kutoka kampuni ya Sanaria, Rockville.
Baadhi ya watafiti hao wameeleza shauku ya kutaka kujua namna chanjo hiyo itakavyotumika kwa watoto wadogo na kama haitamwondolea kinga nyingine za mwili.

Source: ippmedia.com
No comments:
Post a Comment