Kama wewe ni msomaji mzuri wa makala za afya basi hautapingana na mimi kwamba kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita dunia nzima ilikuwa imeshtushwa na habari iliyomeki headline kwenye vyombo vingi vya habari ikiwemo 'AFYA YA MAZINGIRA' kwamba kirusi kinachoambukizwa kwa ngono zembe (including Oral sex) cha Human Papilloma Virus (HPV) kinaweza kusababisha Saratani ya Kinywa. (bofya hapa)
Pamoja na habari hiyo, leo nakuletea mpya nyingine inayohusu utafiti uliochapishwa kwenye Jarida la tafiti za kuzuia saratani (Cancer prevention research jornal) ambao umeonyesha kwamba afya duni ya kinywa na magonjwa ya fizi yanaweza kurahisisha maambukizi ya HPV na hivyo kupelekea Saratani ya Kinywa.
Utafiti huo uliofanywa na watafiti kutoka chuo kikuu cha sayansi za afya cha Texaz kilichipo mjini Hauston, ulijumuisha watu 3,400 waliokuwa na umri wa kati ya miaka 30 na 69. Watu hao waliojumuishwa kwenye utafiti huo walitakiwa kutoa taarifa zao za afya ya kinywa na hali zao (status) za maambukizi ya HPV.
Wale wote walioripotiwa kuwa na afya duni ya kinywa walikuwa kwenye hatari kubwa ya kuambuzwa HPV kwa asilimia 56 ukilinganisha na wale waliokuwa na afya bora ya Kinywa. Pia wale wote walioripotiwa kuwa na magonjwa ya fizi na matatizo mengine ya meno walikuwa kwenye hatari ya kuambukizwa HPV kwa asilimia 51 ukilinganisha na wale waliokuwa na afya bora ya kinywa.
Watafiti waliyaelezea matokeo ya utafiti huo kuwa yanaweza kubadilika na jamii inaweza kujikinga na maambukizi ya HPV ikiwa kama watu watasukutua/watapiga mswaki vizuri kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya (angalau mara tatu kwa siku baada ya milo ya asubuhi, mchana na jioni) na kuhakikisha mazingira ya kinywa yanakuwa safi muda wote.
Pamoja na ushauri huo lakini pia watafiti wameelezea faida zingine ambazo mtu mwenye afya bora ya kinywa anaweza kuzipata ikiwa ni pamoja na kujikinga na magonjwa ya fizi mfano ugonjwa wa Gingivitis ambao unahusishwa na kusababisha ugonjwa wa Moyo.
Takwimu zinaonyesha kwamba kwa Marekani pekee wanawake takribani 2,370 na wanaume 9,356 hupata saratani ya kinywa inayotokana na HPV kila mwaka.
Source: CNN
No comments:
Post a Comment