Wanasayansi na watafiti nchini Uingereza wamevumbua nguvu
za mkojo katika kuzalisha nishati ambayo inaweza kuchaji simu kwa muda wa
dakika 25 na pia kumwezesha mteja kutuma ujumbe na kuperuzi intaneti.
Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Watafiti cha
Bristol wakishirikiana na wenzao wa Maabara ya Robot wanasema kuwa nishati hiyo
ya mkojo ni mapinduzi ambayo yatasaidia katika upungufu wa nishati wakati
wowote badala ya kutegemea jua au upepo.
Timu ya watafiti hao iliweka mkojo katika chombo
maalumu ambao baada ya muda ulizalisha bakteria.
Bakteria hao baada ya kuwa na njaa huzalisha nguvu
za kielektroni na kuwa nishati. Elektroni hizo hudondoshwa katika kontena
maalumu kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Mmoja wa wahandisi aliyevumbua nguvu za mkojo, Dk
Ioannis Ieropoulo wa Chuo Kikuu cha West of England (UWE), Bristol
anasema, mkojo ni bidhaa ambayo haiwezi kutupungukia tofauti na bidhaa nyingine
kama maji, upepo au jua.
Wavumbuzi hao wanasema mkojo ni nishati inayopatikana
wakati wowote hivyo hatua hiyo inasaidia kuwa na uhakika wa kutopungukiwa na
nishati hata kwa watu wa vijijini.
Anaongeza kuwa madhumuni ya uvumbuzi huo ni kupata
nishati inayopatikana wakati wowote, rahisi kuiunda na itakayowasaidia watu
wengi wa matabaka mbalimbali.
“Tumevumbua na tumehakikisha kuwa inafanya kazi.
Kilichobaki sasa ni kuangalia uwezekano wa mkojo kutumika katika matumizi ya
nyumbani,” anasema mhandisi huyo.
Mpaka sasa betri iliyoundwa kwa nishati ya mkojo huo ina
uwezo wa kuchaji simu itakayoweza kudumu kwa dakika 25, kutuma ujumbe na kupiga
simu kwa sekunde 20.
Kutokana na matokeo mazuri ya utafiti huu ni wazi kwamba kama teknologia hii itaingia kwenye nchi zetu zinazoendelea kama Tanzania basi itasaidia kwa kiasi kikubwa kunusuru uharibifu wa Mazingira unaofanywa na watu wanaokojoa hovyo katika sehemu zisizohusika lakini pia itasaidia kupata nishati mbadala na endelevu kwa watu wa Maisha ya Chini na ya kati.

Source: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment