Mabadiliko ya hali ya
hewa yamekuwa yakielezwa kusababisha mabadiliko ya ghafla ya majira, kuyeyuka
kwa barafu na kupanda kwa kina cha bahari. Lakini tumesahau madhara makubwa ya
kuenea kwa magonjwa ambayo yanaweza kutokea kwa binadamu, mimea na wanyama.
Kuongezeka kwa joto
kuna badilisha mazingira yetu kwa kuondoa ulinzi wa asili dhidi ya magongwa na
hivyo kuvifanya vimelea vya magonjwa kuishi maisha marefu yenye mafanikio tele.
Dalili kubwa tunaweza
kuziona kwenye maeneo ya baridi ya pembezoni mwa dunia (North Pole), ambapo imeripotiwa
kuongezeka kwa minyoo (parasitic worms) inayoathiri wanyama wa huko (musk ox na
reindeer) na athari hizo zinaonekana kusambaa kwa kasi maeneo mengine.
Ukanda wa joto kama
vile visiwa vya Caribbean umeripotiwa kuongezeka kwa joto linaloathiri
mahusiano ya viumbe vya majini (symbiosis) na kuvifanya viumbe hivyo viwepo
hatarini kupata magonjwa. Pamoja na kuwepo na athari kwenye mahusiano hayo lakini
pia imeripotiwa kuwepo kwa ongezeko la ukuaji wa bacteria hatari kwenye ukanda
huo.
Katika nchi
zinazoendelea (ikiwemo Tanzania) kumekuwapo na ongezeko la vimelea (pathogens)
ambavyo vimekuwa vikiathiri kilimo na viumbe mwitu (wildlife) na hivyo
kuhatarisha usalama wa chakula na maisha ya watu waishio maeneo hayo.
USHAURI: Ili kujikinga
na magonjwa ya binadamu yanayoweza kuchochewa na mabadiliko ya hali ya hewa, serikali
inapaswa kuwaongezea nguvu wadau wa afya wanaojishughulisha na ufuatiliaji wa
magonjwa (disease surveillance), udhibiti wa wadudu waenezao vimelea vya magonjwa
(vector control), usafi wa mazingira (waste management and sanitation), Madawa
(Drugs), Chanjo (Vaccines), Usalama wa Chakula (food safety and security) na shughuli zingine za KINGA.
No comments:
Post a Comment