Utafiti uliofanyika kwenye
mji wa Charlottesville nchini marekani umebaini kwamba watoto walio na umri wa
chini miaka mitano wanaokunywa vinywaji vya sukari kila siku wako hatarini kuwa
na uzito uliopitiliza (utapiamlo) ukilinganisha na wale wanaokunywa vinywaji
hivyo mara chache au kutokunywa kabisa.
Dk. mark de Bour wa chuo
kikuu cha Virginia ambae alioongoza utafiti huo alisema yeye pamoja na watafiti
wenzake walifanya utafiti kwa wazazi wa watoto 9,500 waliozaliwa mwaka 2001
ambapo umri wa watoto waliofanyiwa utafiti ulikuwa ni miaka miwili, mine na
mitano. Utafiti huo ulizingatia kiwango cha uchumi na elimu cha wazazi na muda ambao
watoto hao hupewa vinywaji vya sukari na kuangalia luninga. Watoto pamoja na
wazazi wao walipimwa uzito wakati utafiti ulipokuwa ikiendelea.
Utafiti huo uligungua
kwamba uwiano (propotional) wa watoto wanaokunywa japo soda moja kwa siku na
vinywaji vingine vya sukari ulikuwa ni kati ya 9% hadi 13% kutegemea na umri
wao.
baada ya utafiti huo
watafiti walibainisha kuwa watoto wenye umri wa miaka mitano wanaokadiliwa kunywa angalau soda moja kwa siku walikuwa ni
sawa na asilimia 43%, walikuwa hatarini zaidi ya kupata utapiamlo ukilinganisha na watoto
wanaokunywa vinywaji vya sukari mara chache au kutotumia kabisa.
Na watoto wa miaka minne
ambao wameripotiwa kunywa vinywaji vya sukari kwa wastani walionekana kuwa wengi
wao wana uzito uliopitilza kuliko watoto wasiotumia.
Utafiti huo haukuonesha
uhusianao kati ya matumizi ya vinywaji vyenye sukari na kuzidi kwa uzito kwa
watoto walio chini ya miaka miwili. Hali iliyohitimisha kuwa matumizi ya
vinywaji vya sukari kwa watoto chini ya miaka mitano yanaleta utapiamlo kwa
kadri muda wa matumizi ya vinywaji hivyo unavyoongezeka.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment