Published by MWANANCHI
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Isaya Mzoro akiwaeleza jambo waandishi wa habari kuhusu utendaji na mipango ya taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
Miezi 10 baada ya kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa
Bohari ya Dawa (MSD), Joseph Mgaya kwa tuhuma za kusambazwa kwa dawa bandia za
kupunguza makali ya Ukimwi (ARV’s), uongozi wa bohari hiyo jana umeibuka na
kusema kuwa umejipanga kuhakikisha ununuzi wa dawa bandia hautokei tena.
Mbali na kueleza mipango na utendaji wake, bohari hiyo
imekiri wazi kuwa, mahitaji ya dawa nchini ni makubwa ikilinganishwa na bajeti
inayotolewa na Serikali, kwamba mwaka jana ilihitajika Sh189 bilioni za kununua
dawa lakini zilipatikana chini ya Sh100 bilioni.
Imesema tatizo hilo linachangiwa na bajeti finyu, pamoja
na uhaba wa viwanda vya kuzalisha dawa nchini, huku ikieleza kuwa kwa sasa kuna
viwanda vitatu tu vinavyozalisha dawa nchini. Vingine vikiwa vimefungwa ama
kuzalisha dawa za kutibu magonjwa ya aina moja tu.
Akizungumza na Mwananchi mara baada ya kumalizika kwa
mkutano wake na wanahabari jana kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, Kaimu
Mkurugenzi wa Bohari hiyo, Isaya Mzoro alisema hivi sasa wamekiimarisha Kitengo
cha Usimamizi wa Ubora wa dawa na kwamba kinafanya kazi zake vizuri, kwa
ukaribu mkubwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
“Tumekuwa na mikutano kati yetu na TFDA ili kuhakikisha
kwamba tunadhibiti ubora wa dawa zinazowafikia Watanzania,” alisema.
Alipoulizwa kwa nini bohari hiyo ilinunua dawa bandia
ambazo hazikuwa na ubora unaotakiwa alisema, “Hilo suala sitapenda kulisema
hapa kwa sababu linashughulikiwa na vyombo vya sheria, usalama wa taifa na
polisi, ila kwa sasa kitengo cha usimamizi na ubora wa dawa kimeimarishwa.”
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment