Ungonjwa wa mafua ya
ndege unaosababishwa na kirusi aina ya H7N9 ambao awali ulilipotiwa kusambazwa
kutoka kwa ndege mwenye ugonjwa huo kwenda kwa binadamu, sasa unasadikiwa
kusambazwa kutoka kwa binadamu aliyeambukizwa kirusi hicho kwenda kwa binadamu
mwingine kwa njia ya hewa.
Uwezekano huo umekuja
miezi miwili tangu kuripotiwa kutokea kwa Ugonjwa huo baada ya mwanamke moja
(32) nchini china kusadikiwa kuambukizwa virusi vya ndege (H7N9) kutoka kwa
Baba yake mzazi, inasemekana Baba huyo (60) alienda kutembelea soko la ndege na
baada ya wiki moja alipata mafua makali ambapo mtoto wake wa kike alilazimika
kumbeba na kumpeleka hospitalini, walipofika hospitalini walipimwa na
kugundulika kwamba wote wameambukizwa mafua ya ndege na hivyo kulazwa kwenye
chumba cha wagonjwa walio chini ya uangalizi maalumu (ICU), baadae wote wawili
wakafa kutokana na kufeli kwa viungo vya ndani (multiple organ failure).
Baada ya tukio hilo Wataalamu wa Afya walichukua vipimo vya watu 43 waliowahi kuwa karibu na wagonjwa wa mafua ya
ndege (H7N9) lakini matokeo yalikuwa ni ‘NEGATIVE’, na hivyo kuonyesha kwamba
uwezo wa kirusi hicho kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine ni
mdogo.
Mpaka sasa hakuna uthibitisho
wa kiutafiti unaoonyesha kwamba kirusi hicho (H7N9) kinaweza kujibadili na
kupata uwezo wa kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Hivyo tukio
lililotokea ni la kwanza kutokea na linaonesha huenda kuna uwezekano wa
kusambaa (probable transmission) kwa virusi hivyo (H7N9) baina ya watu kwa njia
ya hewa.
Ugonjwa wa mafua ya
ndege (H7N9) uliripotiwa na Shirika la Afya duniani (WHO) kutokea nchini China
tarehe 1 mwezi wa 4 mwaka huu, ukitokea kwa wanyama aina ya ndege. Tangu kutokea
kwa ugonjwa huo, zaidi ya watu 130 wameripotiwa kuambukizwa virusi vya H7N9 na
40 tayari wameshapoteza maisha yao mpaka sasa.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment