UGONJWA WA MAFUA YA NDEGE WAUWA MTU MWINGINE



Vyombo vya habari nchini china vimeripoti kutokea kwa kifo cha mtu mwingine kilichotokana na aina mpya ya ugonjwa wa mafua ya ndege ambapo mpaka sasa idadi ya vifo kwa ugonjwa huo imefikia watu 44.


Habari za kuaminika kutoka nchini humo zinasema mtu huyo mwenye umri wa miaka 61 kutoka jimbo la kaskazini mwa china, hebei, amefariki dunia siku ya jumatatu (jana) kutokana na viongo vya ndani kushindwa kufanya kazi (multiple organ failure), kabla ya kufa mtu huyo alipimwa mnamo tarehe 20 mwezi wa 7 na kugundulika ana virusi vya ugonjwa huo (H7N9 virus).

Mpaka sasa idadi yawatu walioripotiwa kuambukizwa ugonjwa huo nchini china imefikia 134.

Ugonjwa huu mpya wa mafua ya ndege (H7N9)  ulioikumba China inasemekana kuwa ni hatari na unaoua kwa haraka zaidi ukilinganisha na ugonjwa wa mafua ya ndege unaoenezwa na virusi vya H5N1ambao umeua zaidi ya watu 360 ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita. Imesemekana kirusi hiki kipya (H7N9) kinaweza kujibadilisha (mutate) and kupata uwezo wa kusambaa kiurahisi.

Mwanzoni mwa mwezi huu wanasayansi walitoa ripoti ya kesi (case) ya kwanza ya uwezekano wa kusambaa (probable case) kwa kirusi hiki cha H7N9 kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine tofauti na mwanzo ambapo ilifikiriwa kwamba kirusi hiki kina uwezo wa kutoka kwa ndege peke yake kwenda kwa binadamu.


Source: VOA



No comments:

Post a Comment