Utafiti wa watoto
625,000 uliochapishwa kwenye jarida JAMA pediatrics nchini Marekani umebaini
kwamba watoto ambao mama zao walitumia madawa ya kuongeza uchungu/kusaidia
uzazi wakati wa kujifungua wako hatarini
kupata ugonjwa wa upungufu wa akili ambao kwa kitaalamu unajulikana kama Autism.
Utafiti huo uliofanyika
kwenye jimbo la Carolina kaskazini umeonyesha kwamba watoto wa kiume13 kwa kila
watoto 1,000, na watoto wa kike wanne kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa na wamama
wanaotumia madawa ya kuongeza uchungu/kusaidia uzazi wakati wa kujifungua, hupata
ugonjwa wa Autism.
Utafiti huo pia umeonyesha
kiwango cha kupata Autism (Rate) kwa watoto wa kiume ambao mama zao hutumia
dawa hizo za kusaidia uzazi ni kukubwa mara tatu zaidi ya watoto wa kike.
Hata hivyo watafiti wa
utafiti huu wamesema kwamba kesi (case) za Autism kwa kila watoto 1,000
wanaozaliwa zinaweza kuepukika iwapo wazazi wao wataacha kutumia madawa ya
kuongeza uchungu/kusaidia uzazi. Lakini pia wameonya kwamba kwa kufanya hivyo
kunaweza kusababisha gharama kubwa kwa kuwa madawa hayo husaidia katika uzazi
salama ambao huokoa maisha ya mama na mtoto.
Utafiti huo umekosolewa
vikali na wanasayansi wengi kwa kuwa madawa ya kuongeza uchungu wakati wa
kujifungua yanaokoa maisha ya mama na mtoto na iwapo madawa hayo hayatatumika
basi kuna uwezekano wa kumpoteza mama au mtoto au wote wawili na hivyo kuomba
tafiti zaidi ziendelee kuchunguza sababu hasa za Autism.
Watoto wenye autism huonesha
dalili za kutokuwa na tabia za
kujichanganya na watoto wengine, kutokuwa na mawasiliano ya njia za
maneno na vitendo, kuwa na tabia zinazojirudiarudia n.k. Autism imekuwa ikiaminika kusababisha na mwingiliano
wa kifamilia, matatizo ya kurithi (genetic risks) na matatizo yanayojitokeza
kwa mama wakati wa ujauzito au matatizo yanayojitokeza wakati mtoto anapokua.
Source: BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment