Wazee wenye matatizo ya
mzunguko hafifu wa damu kwenye ubongo wamejikuta katika furaha kubwa baada ya
kupona matatizo yao. Uponyaji huo umetokea baada ya utafiti mpya kubaini tiba
dhidi ya matatizo hayo kwa wazee ikiwa ni pamoja na kunywa vikombe viwili tu vya
kakao (cocoa) kila siku kwa muda wa mwezi mmoja.
Awali utafiti
uliofanyika miaka ya nyuma na kuchapichwa kwenye makala za Neurolojia
ulionyesha kwamba ubongo hufanya kazi yake vyema ikiwa kuna mzunguko mzuri wa
oxygen na sukari kwenye damu, hivyo matatizo ya mzunguko hafifu wa damu kwenye
ubongo baina ya wazee yanasababisha uhaba wa oxygen na sukari kwenye ubongo,
ubongo unaposhindwa kufanya kazi yake vyema husababisha matatizo mengi ikiwa ni
pamoja na tabia ya kupoteza kumbukumbu.
Matokeo ya utafiti
uliyofanywa hivi karibuni yameonyesha kwamba kakao ina uwezo wa kuboresha
mzunguko wa damu kwa watu wenye mzunguko mdogo wa damu hasa hasa wazee, wazee
waliojumuishwa kwenye utafiti huo wameonekana kuimarika uwezo wao wa kufikiri
na kukumbuka hali inayoashiria kakao kuongeza mzunguko bora wa damu kwenye
ubongo. Pamoja na mafanikio hayo lakini utafiti huu umebaini kwamba watu ambao
tayari wana mzunguko mzuri wa damu hawawezi kuboresha uwezo wao wa kufikiria na
kukumbuka kwa matumizi ya kakao.
Wakiongea na vyombo vya
habari, watafiti wa utafiti huu ambao ulijumuisha wazee 60 wenye wastani wa
umri wa miaka 73, walihitimisha kwamba hata kakao yenye kiasi kidogo sana cha flavanols
(kemikali inayopatikana kwenye miti ya kakao) inaweza kuleta mabadiliko makubwa
kwa watu wenye matatizo ya mzunguko hafifu wa damu na kuonya kwamba watu
wasikimbilie kwenye chocolate za cocoa wakidhani kwamba itakuwa mbadala tosha
wa kakao (cocoa).
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment