Utafiti wa kubaini
kinga ya ugonjwa hatari wa ‘uvimbe wa joints’ kwa kitaalamu hujulikana kama
Rheumatoid arthritis, umekuja na matokeo ambayo wengi hawakuyategemea kwamba
kwa kula kipande kimoja cha samaki wa mafuta (oily fish) aina ya Salmon au
Mackerel, inaweza kuondoa hatari zote za mtu kupata ugonjwa huo.
ugonjwa wa Rheumatoid arthritis ulioshambulia joints za mikono
Utafiti huo uliofanyika
nchini sweeden kwa muda mrefu wa takribani miaka kumi, ulijumusiha idadi ya w anawake
(sample) zaidi ya 30,000 ambapo baada ya utafiti kumarizika, imebainika kwamba
wanawake waliokula samaki mzima wa aina
yoyote angalau mara moja kwa wiki walipunguza hatari ya kupata ugonjwa wa ‘Rheumatoid
arthritis’ mara tatu zaidi.
Wale waliokula angalau
kipande kimoja cha samaki wa mafuta (oily fish) au milo mine yenye vipande vya
samaki aina nyingine kila wiki walipunguza hatari mara 0.5 zaidi ya kupata
ugonjwa wa ‘Rheumatoid arthritis’.
Watafiti wanasema mlo
wa samaki ni muhimu sana kwakuwa umesheheni virutubisho vya Omega-3 ambavyo ni
muhimu pia katika ulinzi wa Moyo na Ubongo.
Pamoja na matokeo ya
utafiti huo, watafiti hawakutilia maanani virutubisho vya mafuta ya samaki vinavyotengenezwa viwandani
(Fish oily supplements) lakini wataalamu wengine wamesema kwamba virutubisho
hivyo pia vina umuhimu wa kupunguza hatari ya kupata ugonjwa huo.
Akiongea na vyombo vya
habari, mkurugenzi wa tafiti za tiba ya Arthritis UK, Prof Alan Silman amesema “utafiti
huo unashauri kwamba kula kiasi kikubwa cha mafuta ya samaki inaweza kukinga
uvimbe kujitengeneza kwenye Joints kwa kiasi kikubwa, lakini changamoto ipo
kwenye kubadilisha milo iliozoeleka kwa watu”.
ugonjwa wa Rheumatoid arthritis ulioathiri joints za miguu
Ugonjwa wa ‘Rheumatoid
arthritis’ ni ugonjwa hatari sana unaoathiri zaidi ya watu 580,000 uingereza na
wales (sina Takwimu za Tanzania), jinsi ugonjwa unavyozidi kujitokeza kwa mtu,
kinga ya mwili (immune system) hupambana na Joints na kupelekea kuvimba
(swollen), kukakamaa (stiff) na kupata maumivu makali (painful) kwenye joints.
Source: BBC News
Kusoma utafiti huo BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment