UTAFITI WAGUNDUA ONGEZEKO LA VICHAFUZI HATARISHI KWENYE VISIMA VILIVYOPO KARIBU NA MACHIMBO YA GESI ASILIA



Utafiti uliofanywa kwenye mchanga wa maji ya visima 100 vya watu binafsi karibu na eneo la machimbo ya gesi asilia mji mdogo wa Barnett-Texas, Marekani umegundua kuwepo kwa ongezeko la vichafuzi hatari kama vile arsenic na selenium kwenye visima hivyo.

Watafiti wa utafiti huo wanaamini kwamba kuongezeka kwa vichafuzi hivyo ambavyo ni hatari sana kwa afya ya binadamu vinaweza kuwa vimetokana na sababu nyingi ikiwa ni pamoja na mapungufu yanayojitokeza kwenye viwanda vya kuchimba gesi asilia kama vile kuharibika kwa vifuniko vya visima vya mafuta kutokana na mtikisiko wa kazi za uchimbaji, kushuka kwa tabaka la maji ardhini (water tables) kutokana na ukame au utoaji wa maji arthini unaofanywa wakati wa utoboaji wa miamba kuyatafuta Maji.

Akiongea na vyombo vya habari, kiongozi wa utafiti huo, Prof. Kevin Schug amesema vichafuzi hatari/metali nyingi hupatikana kwenye kina kifupi ndani ya ardhi lakini uharibifu unaofanywa na shughuli za uchimbaji wa gesi asilia unaweza kusababisha vichafuzi/metali hizo kupanda hadi juu ya ardhi.

“utafiti huu hauwezi kutoa hitimisho la sababu za kuongezeka kwa vichafuzi hatari kwenye maji ya visima vya maeneo ya karibu na machimbo ya gesi asilia lakini utasaidia kutoa mwanga kwa tafiti zingine zitakazofuata”. Alisema mmoja wa watafiti hao.

Kusoma zaidi BOFYA HAPA

My take: Hii inatoa tahadhari kwa mataifa mengi ikiwemo Tanzania yanayotaka kuingia kwenye miradi ya uchimbaji wa gesi asilia. nawashauri watu wanaofanya tathmini ya athari za mazingira (EIA) wawe makini kumonitor mabadiliko yatakayojitokeza mara baada ya miradi kuanza ili kuchukua hatua stahiki mapema kabla ya madhara kuwa makubwa.


`

No comments:

Post a Comment