BAGAMOYO KUPIMA UKIMWI NYUMBA HADI NYUMBA



Wakazi wa Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani sasa wataanza kupimwa virusi vya Ukimwi nyumba hadi nyumba.

Akizungumza na NIPASHE, Mratibu wa kudhibiti Ukimwi wilayani humo, Kusena Job, alisema kuwa njia hiyo itasaidia watu wengi kujitambua afya zao.

Hata hivyo alisema zoezi hilo litakuwa la hiyari kwa kumshauri mlengwa. "Tuna mpango wa kuhamasisha upimaji wa Ukimwi kwa kupita nyumba hadi nyumba hii itasaidia kila mmoja kujitambua afya yake," alisema.

Aliongeza kuwa ipo changamoto ya baadhi ya watu hasa kinababa, kutokuwa na mwamko wa kujitokeza kupima, ikilinganishwa na kinamama ambao wamekuwa wepesi katika kuitikia hilo.

Alisema kuwa, akinamama hata wanapokuwa wajawazito wanapoanza kliniki, wamekuwa wepesi kukubali kupima na kujitambua.


Bofya HAPA kusoma zaidi




No comments:

Post a Comment