VYOO VYA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI VYATISHA KWA UCHAFU



Wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wako kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa ya milipuko kutokana na vyoo vinavyotumika kukosa maji kwa zaidi ya wiki mbili sasa.

Kutokana na mazingira hayo, ndugu wa wagonjwa hulazimika kwenda na maji kwenye madumu na ndoo kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wao huku wengine wakijaribu hata kufanya usafi kwenye vitanda walikolazwa pamoja na sakafuni.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti la NIPASHE kwa siku nne, umebaini kuwa hali ya usafi kwenye vyoo hivyo ni ya kutisha kutokana na kuzagaa kwa vinyesi huku chupa tupu za plastiki za soda zikiwa zimejazwa kwenye matundu ya vyoo.

Mmoja wa wagonjwa walioko kwenye wodi zilizopo kwenye jengo la Mwaisela, akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina lake gazetini, alisema  ametoka mkoani na hivyo hana ndugu wa kumpelekea maji.

Alisema hali hiyo inamfanya akose hata maji ya kunawa uso na hivyo kuwa ombaomba kwa wagonjwa wenzake.

“Kwa kweli hali ni tete, tangu Julai 15, mwaka huu,  hatuna maji lakini cha kushangaza kila siku wahudumu wanamwagilia maua hapo chini tena yana nguvu kweli kweli,” alisema.

Ofisa Mawasiliano wa hospitali hiyo kubwa kuliko zote nchini, Aminiel Aligaeshi, alikiri kuwapo kwa tatizo hilo huku akisisitiza kuwa jitihada zinafanywa kuhakikisha maji yanapatikana kama kawaida.



Kusoma zaidi BOFYA HAPA



No comments:

Post a Comment