Shirika la Umoja wa Mataifa
linalojishughulisha na magonjwa ya UKIMWI limetoa ripoti ya kile kinachoelezwa
kuwa ni hatua kubwa katika kupambana na magonjwa ya maambukizi ukanda wa mashariki
na kusini mwa bara la Afrika. Ripoti hiyo imeonesha kupungua kwa kiasi kikubwa
cha vifo vinavyotokana na ugonjwa wa UKIMWI, ripoti hiyo pia imeonesha kupungua
kwa maambukizi mapya ya UKIMWI lakini imeonya kwamba changamoto za kupambana na
Ugonjwa huo hatari bado zinawakabili.
Vyombo vya juu vya afya
duniani vimeisifu hatua hiyo kubwa ya kupambana na UKIMWI ukanda wa mashariki
na kusini mwa Afrika, Vifo vinavyotokana na UKIMWI vimeshuka kwa asilimia 40 tokea mwaka 2005, na maambukizi
mapya ya UKIMWI kwa watoto yameshuka kwa asilimia 50 tangu mwaka 2001.
Sababu kuu ya kushuka
kwa Vifo hivyo ni kuongezeka kwa watu wanaotumia Dawa za kupunguza makali ya
Virusi vya UKIMWI (ARV), kutoka watu 625,000 mnamo mwaka 2005 hadi kufikia watu
milioni 6.3 mwaka 2012.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment