Na: ROSE RIWA
Hivi karibuni nchi
zinazoendelea zimegubikwa na wimbi kubwa sana la matumizi ya technologia
mbalimbali katika maisha ya kila siku ikiwepo matumizi ya simu na mitandao
mbalimbaili.
Teknolojia ya simu
hutumia mionzi ya masafa marefu ambayo inajulikana kwa lugha ya kitaalamu kama “wireless
microwave radation”, techinologia hii inaendelea kwa kadri siku zinavyozidi
kwenda na watu wengi wanapendelea na kukimbilia kuishi sehemu zenye mtandao kwa
sababu za urahisi wa kimawasiliano.
Mawasiliano hayo ya simu usafiri toka sehemu
moja kwenda sehemu nyingine kwa njia ya minara ya simu. Sehemu yoyote ile ambayo unaoweza kupiga au
kupokea simu tambua kunamtandao
unaosambazwa na minara hiyo.
Sehemu ambazo minara ya
simu imeonekana kuwa na mionzi mikali zaidi ni milimani na kwenye miinuko nje
ya miji. Mionzi hii ina madhara kwa binadamu,mimea na viumbe hai vingine kama
wanyama sababu hupata dozi ya moja kwa moja
kutokana na kukosekana kwa vizuizi” obstruction/ barriers” hali inayofanya mionzi
kusafiri moja kwa moja kutoka kwenye chanzo hadi kwa viumbe hai, na hii hupelekea kiwango cha dozi ya mionzi kuwa kikubwa kwa muda mrefu.
Mionzi hii inauwezo wa
kusafiri katika umbali wa kuanzia mile 2
katika miinuko hadi miles 45 katika sehemu zenye vizuizi vichache(barrier) na
ina uwezo wa wa kupenya hata kwenye ukuta na chuma. Minara hii inakuwa ni
hatari zaidi endapo itatoa mionzi zaidi ya 1900 MHz. na hii imeonyesha kuwa na
athari kwa viumbe hai wakiwemo banadamu wanaoishi ndani ya kilometa moja kutoka
kwenye chanzo.
Pamoja na hayo ni vigumu kukimbia mionzi hiyo sababu ipo
kila sehemu yenye mawasiliano japo nguvu ya dozi inapungua kulingana na umbali
wa chanzo na watu,, kuwepo kwa vizuizi kama vile majengo ambayo yanauwezo wa
kupunguza nguvu ya mionzi hiyo na kupunguza muda wa dozi husika.
Aidha tafiti mbalimbali
za nchi zilizoendelea zimebainisha kuwa vuimbe hai vinavyoishi sehemu hizo vipo
kwenye hatari zaidi ya kupata dozi kubwa ya mionzi hiyo. Mwili wa bianadamu
wenyewe unauwezo wa kutoa dozi ya chini sana ya mionzi kama 10hertz, na kila
chembechembe ya mwili wetu ina mionzi yake ( cellular electromagnetic field) ,Watafiti
wamesema frequency za kutengenezwa zinazozidi
10 hertz zinaweza sababisha msongo wa
mawazo, matatizo ya kukosa usingizi, matatizo ya kizazi na saratani mbailimbali
endapo binadamu atapata dozi hiyo kwa muda mrefu.
Minara ya simu ina
mionzi yenye nguvu zaidi kulinganisha na mionzi ya radio (the higher the
frequency the more powerful the wave = more powerful effects on biological organisms)
na kumbuka mionzi ya minara ya simu ina nguvu 1900 MHz. Mionzi hii inauwezo waa
kuharibu bond ya molekula na chemicali na kusababisha mabadiliko ya vinasaba (DNA),
Metabilism,vichocheo vya mwili (hormones) na enzyemes hali inayopelekea madhara
yafuatayo ya kiafya:
1. Kuumwa kichwa(headache)
2. Kukosa kumbukumbu(memory loss)
3. Kupungua kwa mbegu za kiume za uzazi
(low sperm count)
4. Saratani na kasoro za uzazi
5. Matatizo ya moyo
6. Msongo wa mawazo
7. Kukosa usingizi.
Kibaya zaidi mionzi hii
ina tabia ya kujilimbikiza kwenye mwili (body accumulation) na kuja kuonesha
madhara miaka kadhaa inayofuata kutegemea na mtu na mtu na hali ya afya ya mtu.
No comments:
Post a Comment