Imerekebishwa na kuchapishwa kutoka Gazeti la Habari leo, Tarehe 12/07/2013
Utafiti wa kisayansi,
haujabainisha athari za kiafya zinazoweza kujitokeza kwa ulaji wa unga na
majani ya mbuyu, isipokuwa kwa mafuta yatokanayo na mbegu za mti huo. Mamlaka ya
chakula na dawa (TFDA) imesisitiza kwamba mafuta hayo ni hatari ikisema yana
kiwango cha tindikali ya mafuta ya cyclopropenoic.
TFDA katika taarifa
yake ya ufafanuzi iliyotolewa jana, ilisema kiwango cha tindikali hiyo huweza
kuondolewa katika mafuta hayo kwa kuyachemsha kwa kiwango cha nyuzi joto 180o
kwa saa nane, au kutumia teknolojia ya
kuyagandisha.
“kwa sasa nchini,
hakuna aina ya usindikaji unaofanyika wenye uwezo wa kuondoa tindikali ya
cyclopropenoic katika mafuta ya ubuyu”. Ilieleza taarifa hiyo. Iliendelea kusema,
hadi sasa hakuna kiwango chochote cha ubora na usalama cha kitaifa au kimataifa
cha mafuta yatokanayo na mbegu za ubuyu.
“ili kuepuka athari
zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya mafuta hayo, jamii inashauriwa
kuepuka ulaji wake”. Ilisisitizwa taarifa hiyo. Mamlaka hiyo pia ilitoa mwito
kwa wananchi na jamii kushirikiana kulinda afya za walaji kwa kutoa taarifa
wanapouziwa au kuhisi kuwepo kwa chakula, dawa, vipodozi na vifaa duni na
bandia, ambavyo havikidhi viwango vya usalama na ubora.
Bofya HAPA uisome zaidi!
No comments:
Post a Comment